Mchezaji wa timu ya Darts ya Jeshi la Polisi Tanzania inayoshiriki michezo ya SARPPCO 2025 nchini Ethiopia, Sgt David Timothy Lyanga ameibuka mshindi wa pili katika mchezo huo na kunyakua medali ya fedha huku timu ya Darts ya Jeshi la Polisi Tanzania ikiibuka mshindi wa tatu na kujinyakulia medali ya shaba katika Mashindano ya Michezo ya EAPCCO 2025 yanayoendelea leo tarehe 01/05/2025 katika uwanja wa Abebe Bikila Stadium jijini Adidas Ababa nchini Ethiopia ikiwa ni siku ya Tano ya michezo hiyo.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Leonard Ngasa, Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Jeshi la polisi amewaongoza wanamichezo wa Jeshi la Polisi Tanzania wanaoshiriki michezo hiyo kushuhudia mchezo huo.