Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi amesema Maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Nchi yoyote yanahitaji jamii yenye Watu wenye Afya Bora.
Mama Mariam ambae pia ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Zanzibar Maisha Bora Foundation(ZMBF) amesema hayo alipoizindua Zanzibar Afya Week katika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege , Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 8 Mei 2025.
Amesema Zanzibar Afya Week ni fursa nyengine Muhimu ya Kuhakikisha Wananchi wànapata huduma Bora za Afya ikiwemo Elimu ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa mbalimbali Ikiwemo Kisukari, Presha, Saratani ya Matiti , Macho na Moyo.
Mariam Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar Maisha Bora Foundation imejizatiti kushirikiana na Serikali Kuimarisha huduma za Afya na Kuifanya Zanzibar kuwa na Watu wenye Afya Bora na kituo Muhimu cha Utabibu kinachotambulika.
Aidha, Mariam Mwinyi amesema hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Afya hivi sasa zinaakisi dhamira ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ya kuifanya Zanzibar kutoa huduma za Matibabu, Kupunguza Rufaa za kwenda nje ya Nchi kufuata Matibabu na kupunguza bajeti za Matibabu na Wageni wanaofika Zanzibar Kupata huduma za Uhakika za Matibabu.
Halikadhalika Mariam Mwinyi amefahamisha kuwa kupitia Kampeni ya Afya Bora Maisha bora ZMBF imeweza kuwafikia Wananchi 21, 500 kupitia Kambi nne za Afya kuwapatia Wananchi Elimu ya Afya , Unguja na Pemba
Vilevile Zanzibar Maisha Bora Foundation imefanikiwa kupitia Mpango wa Lishe imeweza kuwafikia Wanawake 2,830 Unguja na Pemba kuwapatia Elimu ya Lishe na Afya ya Uzazi na mama wajawazito huduma za Kliniki.
Kwa upande mwingine Mariam Mwinyi amefahamisha kuwa Programu ya Tumaini Initiative ya ZMBF imeweza kuwafikia Wasichana balehe 8,676 Unguja na Pemba wa Skuli za Msingi na Sekondari na kuwapatia Tumaini kits na Elimu ya hedhi Salama na kuchangia Mahudhurio Skuli na kusoma kwa Waweze kusoma kwa kujiamini.
Mama Mariam Mwinyi amesema Serikali imepiga hatua kubwa katika kuimarisha Hospitali na Vituo vya Afya pamoja na Sera na Teknolojia ya Utoaji wa huduma katika Sekta ya Afya na kuipongeza kwa Mafanikio hayo.
Uzinduzi huo uliambatana na Programu za Lishe Bora 2025, Afya Mama na Mtoto 2025 na Shehia Afya Programu 2025 .