Robert Kardinali Prevost ni mzaliwa wa Chicago nchini Marekani, na hadi kuchaguliwa kwake alikuwa akihudumu kama mkuu wa Dicastery wa kanisa kwa Maaskofu.
Papa Leo XIV mwenye umri wa miaka 69 ametumia muda wake mwingi akitumikia nchini Peru, na ana uraia wa Marekani na Peru.
Kabla ya kutangazwa, majina kadhaa yalikuwa yanatajwa kumrithi Papa Francis kuongoza Kanisa Katoliki.
Baadhi ya majina hayo ni Kardinali Pietro Parolin alikuwa katibu wa mambo ya nje wa Vatican chini ya Papa Francis, na kumfanya kuwa mshauri mkuu wa Papa.
Peter Kodwo Appiah Turkson, Mganda wa kwanza kuteuliwa kuwa kardinali chini ya Papa John Paul II mwaka 2003, alipewa nafasi kubwa na watunga vitabu vya bahati nasibu kabla ya kupiga kura mwaka 2013 ambapo Francis alichaguliwa badala yake.
Kardinali Fridolin Ambongo Besungu anatoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako amekuwa Askofu Mkuu wa Kinshasa kwa miaka saba.
Kardinali Luis Antonio Gokim Tagle alitajwa kama chaguo muhimu. Kanisa Katoliki lina ushawishi mkubwa katika nchi yake ya Ufilipino, ambako takriban 80% ya watu ni Wakatoliki.
Makardinali Robert Prevost na Joseph Tobin, pia walitajwa mara kadhaa kama warithi wanaowezekana.
Mkutano wa siri wa kumchagua Papa ulianza jana katika kanisa dogo la Sistina, ukijumuisha makadinali 133 kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Kuchaguliwa kwa Papa huyu kunafuatia kifo cha Papa Francis, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 88 siku ya Jumatatu ya Pasaka 21 April, na mazishi yake kufanyika siku ya Jumamosi 26 April.
Huu ni mkutano wa tatu wa uchaguzi wa Papa unafanyika kwa siku mbili na kumpata papa. Mikutano mingine ni ile iliyofanyika mwaka 2005 na 2013, ambayo ilidumu kwa siku mbili tu.
……………………
Papa Robert Francis Prevost, anayejulikana rasmi kama Papa Leo XIV,
ni kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani kuanzia Mei 8, 2025.
Ni Papa wa 267 katika historia ya Kanisa. Ni mara ya kwanza kwa raia wa Marekani kuchaguliwa kuwa Papa.
Jina kamili: Robert Francis Prevost
Tarehe ya kuzaliwa: 14 Septemba 1955
Mahali: Chicago, Illinois, Marekani
Uraia: Mmarekani na Mperu (alipata uraia wa Peru kutokana na kazi zake za
kimisionari).
Prevost alijiunga na Shirika la Mtakatifu Augustino mwaka 1977 na kuweka nac
zake za milele mwaka 1981.
Alisoma shahada ya kwanza ya Hisabati katika Kikuu cha Villanova, na baadaye kupata shahada ya uzamili ya Theolojia kutoka Catholic Theological Union, pamoja na shahada ya udaktari wa Sheria za Kanisa) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas Aquinas huko Roma.
Alitumikia kama mmisionari nchini Peru kwa miaka mingi, akihudumu kama paroko, mwalimu wa seminari, na baadaye kuwa Askofu wa Chiclayo kuanzia mwaka 2015
hadi 2023.
Mnamo Januari 2023, aliteuliwa na Papa Francis kuwa Mkuu wa ldara ya
Maaskofu (Dicastery for Bishops), mojawapo ya nafasi zenye ushawishi mkubwa katika Kanisa Katoliki.
Baada ya kifo cha Papa Francis mnamo Aprili 21, 2025, Prevost amechaguliwa kuwa Papa katika raundi ya nne ya upigaji kura.
Alipochaguliwa, alichukua jina la Papa Leo
XIV jina ambalo halijatumika tangu mwaka 1903.
Uchaguzi wake unatarajiwa kuendeleza mwelekeo wa Papa Francis wa kuhimiza
usawa, uwazi, na mageuzi ndani ya Kanisa, huku akizingatia uzoefu wake wa
kimataifa na uongozi wa kiutawala.