NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
KLABU ya Simba imeshindwa kufurukuta ugenini dhidi ya wapinzani wao RS Berkane baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa fainali Kombe la Shirikisho Afrika (1st leg).
Katika mchezo huo timu ya RS Berkane ilionekana kuhitaji mabao mengi kwa haraka ambapo walifanikiwa kwa dakika 15 za mwanzo kupata mabao mawili ambayo yaliwekwa kimyani na kiungo machachali raia wa Senagal Mamadou Camara dakika ya 08′ ya mchezo pamoja na mshambuliaji wa Morocco Ousama Lamlioui dakika ya 15′.
Mamadou Camara licha ya kufunga bao, aliweza kulikamata dimba la kati na kuwapoteza Fabrice Ngoma pamoja na Yusuf Kagoma.
Simba Sc itahitaji mabao 3-0 au zaidi kwenye mchezo wa pili ambao watakuwa nyumbani ili kuweza kuibuka mabingwa wa Shirikisho.