KAMPUNI ya Kubashiri ya Kingbet imezindua rasmi kampeni yake ya CHA KUKALIA ambayo inalenga kuwasaidia wateja wanaocheza mchezo maarufu wa Aviator kujichotea Mkwanja wa maana kila usiku.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 5, 2025 jijini Dar es Salaam amesema kampeni hiyo imeanza leo na itafika tamati Desemba mwaka 2025 ambapo itachukua miezi sita.
Amesema kuanzia saa moja hadi saa nne usiku kila siku, wachezaji wa Aviator watakuwa na nafasi ya kupiga mkwanja maradufu si tu kutoka kwenye ushindi wa kawaida wa kindege, bali pia kutokana na maokoto ya kampeni hiyo.
“Mezani, kuna mgao wa hadi TZS 500,000,000! YES huu ni mwaka wa neema kwa watumiaji wa Kingbet”. Amesema
Amesema kingbet itagawanya mgao huo kwa washindi zaidi ya 3,000 watakaokidhi vigezo kwa kucheza Aviator mara nyingi zaidi kati ya saa 1 hadi saa 4 usiku.
“Washindi watalipwa papo hapo, hakuna kusubiri mpaka asubuhi, Tukisema tunakupa CHA KULALIA, tunamaanisha hautalala mpaka upate ushindi”. Amesema
Aidha amesema Kingbet imetengeneza fursa hiyo kwa kuelewa mapenzi ya wachezaji wake kwa mchezo huo, na sasa imeamua kuugeuza kuwa tobo la mshiko kwa kila mchezaji.
Kwa upande wake Balozi wa Kampuni hiyo, mchekeshaji wa Majukwaa, Neila Manga amesema mgao wa hadi Sh. 500,000,000 uliowekwa ni bonge la shavu kila mtu ana nafasi ya kupata na kila mmoja atapata CHA KULALIA.
“Na ili kuhakikisha kila mmoja anapata, tumerahisisha namna ya kushiriki na kushinda kumerahisishwa sana yaani ukirusha Kindege cha Aviator kuanzia saa moja usiku hadi saa nne usiku basi unajiweka katika nafasi ya kusepa na mgao wa mpaka Sh. 500,000,000”. Amesema