Benki ya NMB imeanza rasmi kutoa huduma zake katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama SabaSaba, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kupitia banda lake maalum, NMB inawakaribisha wananchi, wajasiriamali, pamoja na familia kwa ujumla kupata huduma kamili za kibenki pamoja na elimu ya fedha kwa ajili ya maendeleo yao ya kifedha.
Katika siku za mwanzo za maonesho hayo, wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Gilman Lutihinda walipata fursa ya kutembelea banda la NMB na kufundishwa masuala mbalimbali ya fedha, ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kukuza uelewa wa kifedha kwa vizazi vyote.
NMB itaendelea kutoa huduma kwa siku zote za maonesho, ikiwemo kufungua akaunti papo hapo, kutoa mikopo, bima, huduma za kidigitali kama NMB Mkoni, na ushauri wa kifedha kwa watu binafsi na wafanyabiashara.
Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda la NMB kwa huduma bora, ushauri wa kitaalamu, na suluhisho bunifu zinazobadilisha maisha.