Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amewavisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) maafisa watatu waliopandishwa kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) leo Julai 1, 2025 jijini Dar es salaam.
Maafisa waliopandishwa cheo ni pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Polisi Wanamaji, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Moshi Nsabi Sokoro, Mkuu wa Kikosi cha Matengenezo ya Magari ya Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Tuntufye Absalome Mwakagamba na Mkuu wa Kikosi cha Bendi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Msolo Hamis Msolo.
IGP Wambura amewavisha cheo hicho baada ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kuwapandisha cheo maafisa hao Julai 1, 2025.