IKIWA leo ndiyo siku ya mwisho ya watia nia ya ubunge na udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchukua fomu , Kada wa Chama Benard Mwakyembe, amerejesha fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Temeke.
Mwakyembe ambaye aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Mtoni wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam, alirejesha fomu hiyo kwa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Daniel Sayi.
“Nikipata ridhaa ya Chama kuwania nafasi hiyo na kushinda nitasimamia fursa mbalimbali za vijana pamoja na kuhakikisha mikopo asilimia 10 inayotolewa na halmashauri inawanufaisha vijana, wanawake na wenye ulemavu,”amesema Mwakyembe.
Juni 28 mwaka huu CCM ilifungua dirisha la uchukuaji na urejeshaji fomu ambalo limefungwa rasmi leo saa 10:00 alasili huku ikishuhudiwa idadi kubwa ya wanachama walio tia nia wakichukua na kurejesha fimu katika ofisi za Chama ngazi ya kata, wilaya na jumuia zake.