
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ameshiriki uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 uliofanyika leo, Julai 17, 2025, jijini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi huo, amesema kuwa akiwa Mwenyekiti wa CHADEMA kabla ya kustaafu, chama chake kilishiriki kikamilifu katika kutoa maoni na mawazo kwa ajili ya maandalizi ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.
Amesema kuwa taifa lolote linapojitafutia dira, ni muhimu kuanza kwa kutambua maeneo ambayo limekosea katika historia yake ya maendeleo.
Aidha, Mhe. Mbowe amesema kamati iliyoshiriki kuandaa dira hiyo imefanya kazi kubwa kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo, vyama vya siasa pamoja na taasisi binafsi.
Na Meleka Kulwa – Dodoma