Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) Bi. Shukrani J. Haule amekabidhiwa tuzo ya Mfanyakazi Hodari wa Taasisi katika Mkutano wa Jumuiya za Wataalam wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala katika Utumishi wa Umma Tanzania (TAPA-HR), unaofanyika Jijini Arusha Katika Ukumbi wa kituo cha Mikutano cha kimataifa (AICC).
Bi. Shukrani amekabidhiwa tuzo hiyo leo 23 Julai,2025 na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said.
Mkutano huu umewakutanisha wataalam zaidi ya 900 kutoka Wakala wa Serikali, Taasisi za Umma, Wizara, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao wanasimamia Rasilimali Watu na Utawala.