Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wanachama wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU-PSC) kujadili hali ya usalama nchini Libya.
Mkutano huo umeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Uganda na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, leo tarehe 24 Julai, 2025 kwa njia ya mtandao ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni wa nchi mwanachama wa Baraza hilo ambalo linaundwa na nchi 15 za Umoja wa Afrika.
Katika Mkutano huo, Bashungwa kwa niaba ya Rais Samia amepongeza Juhudi za Mheshimiwa Denis Sassou Nguesso, Rais wa Jamhuri ya Congo na Mwenyekiti wa AU High Level Committee on Libya, hususani kwa kusimamia The National Reconcilliation Charter ambayo inatoa muongozo wa suluhu ya mgogoro nchini Libya ikiwemo kufanyika kwa uchaguzi, kuimarisha taasisi nchini Libya hususan Jeshi.