Na Said Mwishehe,Michuzi TV
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)kimepitisha majina ya wagombea ubunge ndani ya Chama hicho katika majimbo ya mikoa mbalimbali nchini yakiwemo ya majimbo ya Mkoa wa Dodoma huku aliyekuwa Spika wa Bunge Job Ndugai jina lake likiwa miongoni mwa majina yaliyong’ara .
Hata hivyo baada ya majina hayo kupitishwa na Kamati Kuu ya Chama hicho sasa yatakwenda kupigiwa kura za maoni na wajumbe ambao wametajwa kikanuni kupiga kura ili kupata majina matatu na kisha jina moja ndilo litateuliwa kuwakilisha Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Akitangaza majina hayo leo Julai 29,2025 mjini Dodoma Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM CPA Amoss Makala amesema katika Jimbo la Kongwa waliopitishwa ni aliyekuwa Spika na Mbunge wa Kongwa Yustino NDUGAI, Balozi. Emmanuel David Mwaluko Luhembe MBENNAHna Ngaya David MAZANDA.
Wengine ni Deus Gracewell SEIF, Philip Eliud CHIWANGA, Paschal Joseph MAHINYILA, Dkt. Simon Saulo NGATUNGA, Dkt. Samora Stanley MSHANG’A, Isaya Mngurumi MOSES na Elias John MDAO
Katika Jimbo la Bahi waliopitishwa ni Kenneth Ernest NOLLO, Robert Elieza KAMUNYA, Suphian Saidi MASASI, Mathias Paul OLYAMUNDA na Dkt. Frolian Sanya SILANGWA
Kwa upande wa Jimbo la Chamwino ni Deogratius John NDEJEMBI, Pololet Kamando MGEMA, Rehema Elias KAYOMBO, Vicente Antony CHOMOLA, Iddi Shabani MWALUKO na Joel Mwaka MAKANYAGA
Kwa Jimbo la MVUMI ni Livingistone Joseph LUSINDE, Dr. Michael Bedson MSENDEKWA, Happiness William MGONGO, Stephen Anderson ULAYA, Nyemo Gideon MASIMBA, Micky Joel MASANYAJI na Amos Daudi Michael MSANJILA
Wakati Jimbo la CHEMBA ni Kunti Yusuph MAJALA, Amina Hashim BAKARI, Khamis Suleiman MKOTYA, Juma Selemani NKAMIA, Omary Salum FUTO na Francis Mahu JULIUS
Katika Jimbo la KONDOA MJINI ni Ally Juma MAKOA , Mariam Ditopile MZUZURI, Ally Nurdin JUMA (SIX) na Dr.Athumani Ramadhani MCHANA
Kwa upande Jimbo la KONDOA VIJIJINI ni Ashatu Kachwamba KIJAJI, Said Omary MNYEKE, Hassan Juma LUBUVA, Juma Twaha SHABANI na Hans Halifa HIDA
Wakati kwa Jimbo la MPWAPWA ni George Natany MALIMA, Njamasi Simon CHIWANGA, Zakayo Norbert MKEMWA, Adam Michael MALIMA, June Ibrahim FUSSI , Margret Jim LEMA na Eva Adrian MPAGAMA
Kwa Jimbo la KIBAKWE ni George Boniface SIMBACHAWENE, George Andrew KAHELA, Dr. Kwame Daimon MWAGA, Nelson Boniface MNYANYI na Amani James BENDERA