NI majeraha ambayo yalifanya asionyeshe ubora wake akiwa katika uwanja msimu wa 2024/25 na alipata maumivu makubwa kwenye mchezo dhidi ya TaboraUnited alipokomba dakika 10 pekee, Uwanja wa Azam Complex.
Ilikuwa ni Novemba 6 2024 zama za Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Anaitwa Aziz Andambilwe alicheza jumla ya mechi tano za ligi akikomba dakika 125, hakufunga wala kutoa pasi ya bao kiungo ambaye alikuwa anacheza nafasi ya beki wakati mwingine.
Katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Azam Complex alikomba dakika 90 na ubao ukasoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania.
Ilikuwa ni Oktoba 22 2024, mwamuzi alikuwa Ahmed Arajiga, Azam Complex . Ameongeza mkataba wa miaka miwili bado yupo Jangwani kijana mpaka 2027.