……….
Zaidi ya wakazi wapatao 45 wamejitokeza katika kambi ya siku tatu ya upimaji bure wa afya na macho na kukutwa na matatizo ya mtoto wa jicho na kufanyiwa upasuaji katika hospital ya Med Wel iliyopo Kibaha mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Khoja Shia ithninasher Mkoa wa Dar es salaam Alhadji Mohammedraza Dewji amesema kuwa ,katika siku mbili za mwanzo za Kambi ya mafunzo ya Imam Hussein(as) jumla ya wakazi wapatao 45 waliojitokeza katika mafunzo hayo ya kambi ya afya na macho.
Alhadji Mohammedraza ameeleza kuwa watu wengi wamepimwa katika siku hizo za kambi na kukutwa na tatizo la mtoto wa jicho wamefanyiwa upasuaji katika hospital ya med well iliyopo kibaha mkoani Pwani inayomilikiwa na jumuiya ya Khoja Shia ithninasher Mkoa wa Dar es salaam.
Aidha, Mwenyekiti huyo alisema kuwa katika mafunzo hayo mbali na kupimwa macho na kutolewa kwa miwani na dawa pia kulikuwa na huduma za bure za upimaji wa afya na maradhi yasioambukiza kama upimaji wa presha (shinikizo la damu la juu) ,kisukari ,uchanguaji damu salama kwa kushiriiana na mpango wa Taifa wa damu salama na upimaji wa Saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa kina mama na tezi dume kwa wanaume ambalo jumuiya hiyo ndio iliyoratibu shughuli hiyo.
Mwenyekiti huyo, alisema hayo wakati akifunga Kambi hiyo ya upimaji wa Afya na Macho ya siku 3 na kusema kuwa imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na watu wengi kuja kupata huduma ya Elimu ya Mjumkuu wa mtume (SAW) Imam Hussein (as).
Akizuungumza kuhusu kambi ya Afya na macho Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mohammedraza Dewji alisema kuwa kujitolea huko kwa Jumuiya yao ya Khoja Shia Ithnaashari ndio mwanadamu anatakiwa kuishi ivyo na imam Hussein alijitoa ili kuokoa kizazi cha babu yake.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa siku 2 za mwanzo ya kambi hiyo mwamko wa wananchi kuja kupata huduma ilikuwa mkubwa tofauti na Miata iliyopita lakini siku ya mwisho watu zaidi ya 5000 walijitokeza huku uwezo wa kambi hiyo kwa siku ilikuwa kuhudumia wagonjwa wasiozidi 2000.
Alhadji Mohammedraza aliitoa rai kwa wananchi wawe wanajitokeza siku za mwanzo ili kupunguza idadi ya watu kuwa kubwa siku za mwisho wa kambi watakaposikia kuna huduma za upimaji wa Afya na Macho bure basi ni vyema wakafika siku za mwanzo Ili kupata huduma.
“Katika kambi ya safari hii kulikuwa na utofauti na mwaka jana wagonjwa wote waliokutwa na changamoto na mtoto wa jicho na waliokuwa tayari walipelekwa moja kwa moja katika moja ya hospitali zetu ya medwell iliyopo Kibaha mkoani pwani na kwa wengine walipangawa siku ya kwenda kupata matibabu Katika moja ya hospitali zetu za medwell , KSIJ Charitabe Eye Centre kilichopo Temeke” alisema Mohammedraza.
Alisema kuwa Watu wengi sana walijitokeza kupatiwa huduma zao kwani hiyo ni ishara tosha kwamba mwamko ulikuwa mkubwa mno na tumegundua watanzania wengi wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya lakini hawajui kuwa wanaumwa na hawatambui afya zao”, alisema.
Pia, alisema kuwa mbali na kukutwa na changamoto ya mtoto wa jicho pia kuna watu wengine walipima na kukutwa na uono hafifu na kupewa miwani na wengine walipewa dawa za kutibu macho na kwa upande wa maradhi yasiyoambukiza yakiwemo shinikizo la damu Zaidi ya watu.
Vilevile, mwenyekiti huyo alisema kuwa katika tukio hilo pia kulikuwa na zoezi la uchangiaji damu salama na katika zoezi hilo zilikusanywa na zitaweza kuwa msaada tosha kwa wahitaji katika hospital zao.
Mohammedraza alisema kuwa kwa kushirikiana na Hospital ya Taifa na muhimbili kupitia kitengo cha Damu salama na Taasisi ya Kansa ya Ocean road waliendesha zoezi hilo la upimaji kwa wakinamama na walipimwa kansa ya titi walipimwa salatani ya shingo ya kizazi.
“huduma za kuchangia damu salama ni zoezi la kujitolea ambalo linatakiwa liwe kama mazoea kwa kila mtu mwenye sifa ya kuchangia damu aweze kufanya hivyo, kwani zoezi hilo sio la kibiashara bali ni la kwenda kituo cha afya na kuchangia damu, kwani kwenye hospital nyingi Kuna uhitaji mkubwa wa huduma hiyo hususani kwa wakina mama
Kwa upande wake Mkuu wa madaktari katika Kambi hiyo ya Afya na macho Daktari Alihusein Malloo alisema huduma za kuchangia damu salama ni zoezi la kujitolea ambalo linatakiwa liwe kama mazoea kwa kila mtu mwenye sifa ya kuchangia damu aweze kufanya hivyo, kwani zoezi hilo sio la kibiashara bali ni la kwenda kituo cha afya na kuchangia damu, kwani kwenye hospital nyingi Kuna uhitaji mkubwa wa huduma hiyo hususani kwa wakina mama wajawazito na wale waliopata ajali.
Aidha, Dkt.Mallo alisema kuwa pia katika kambi hiyo wako walijitokeza kupatiwa elimu ya afya ya akili, ambayo jamii zetu zoezi hilo ni kama vile limesahulika, kwani ugonjwa huo ambao unakuja kwa Kasi ya hali ya juu limeonekama kuathiri watu wengi sana katika jamii hususani kwa wale wenye msongo wa mawazo pamoja na ule wa kansa ya shingo ya kizazi pamoja na titi .
Dkt. Mallo ameitaka Jamii kuwa na tabia ya kupima afya mara kwa mara na Kuna watu wamekuja apa na kupata Elimu na kujua kuwa Wana matatizo ya afya .
“Kuna watu zaidi ya hamsini watafanyiwa upasuaji wa uvimbe mbalimbali bure bila gharama yoyote.katika Kambi hiyo wamegundua kuwa wagonjwa wengi wamekutwa na matatizo ya macho kutokana na mazingira yanayowazinguka au mazingira ya kazi na kusababisha kuwa na uono hafifu”alisema Dkt. Mallo.
Dkt.. Amesema kuwa Katika Kambi hii tulitegemea kupata watu 4500 kwa siku 3 lakini imekuwa tofauti kwani mwitikio umekuwa mkubwa mno .
Kwa upande wake mmoja wa wafaidika wa kambi hiyo ambaye amepata fursa ya kufanyiwa upasuaji wa mtoto ea jicho Bi Mariam Akida mkazi wa Mbagala jijini Dar es salaam amesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa yenye tija mno kwa upande wake.
Ameendelea kusema kuwa kwa mda mrefu alikuwa na uono hafifu na akujua shida nini na hadi alipokuja kutambua kuwa ana tatizo kwenye jicho .