NA DENIS MLOWE IRINGA
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi Moses Ambindwile ashiriki kupiga kura za maoni kwa nafasi ya Ubunge na Udiwani katika kata ya Mkimbizi .
Katika uchaguzi huo unaofanyika kata kwa kata Ambindwile amepiga kura yake na udiwani majira ya saa saba na nusu huku hali ya utulivu ikiitokeza katika uchaguzi huo wa kata.
Jimbo la Iringa mjini watia nia ya ubunge wako sita ambapo wanaowania nafasi hiyo ni Moses Ambindwile, Jesca Msambatavangu, Islamu Huwel, Nguvu Chengula, Mchungaji Peter Msigwa na Fadhili Ngajilo ambao wanawania nafasi moja ya kuwa mwakilishi wa ubunge katika uchaguzi mkuu wa October 29 mwaka huu.
Naye aliyekuwa diwani wa kata ya Mkimbizi. Eliud Mvela amepiga kura ya maoni kuwania kwa nafasi ya pili ya kuwa mwakilishi katika kata hiyo.


