Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu (kushoto), Afisa Masoko Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Irene Mbonde, na Mkurugenzi wa hospitali ya JKCI-Dar Group, Dk. Tulizo Shem wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa zoezi la kufanya vipimo vya moyo na kutoa elimu ya afya kwa wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania. Zoezi hilo, ikiwa sehemu ya uadhimisho wa miaka 10 ya JKCI, limefanyika katika Makao Makuu ya benki hiyo, Exim Tower jijini Dar es Salaam.
…………
Dar es Salaam, Tanzania: Benki ya Exim Tanzania, taasisi ya kifedha iliyojikita katika ustawi wa jamii, na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), kinara wa huduma za afya ya moyo Afrika Mashariki, wanajivunia kutangaza mpango muhimu wa afya kuimarisha ushirikiano wao. Kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya JKCI, taasisi hiyo imefanya zoezi la upimaji wa magonjwa ya moyo na kutoa elimu kwa wafanyakazi wa Exim Bank Tanzania katika Makao Makuu ya benki, Exim Tower, jijini Dar es Salaam.
Exim Bank Tanzania imeendelea kuonesha dhamira yake thabiti ya kuboresha huduma za afya nchini, ikiwa mmoja wa waungaji mkono wa mwanzo na muhimu wa JKCI. Ushirikiano huu wa kudumu haujaongeza tu juhudi za JKCI za kukuza afya ya moyo nchini, bali pia umekuwa kichocheo kikubwa katika kukuza utalii wa matibabu katika ukanda huu. Uwepo wa benki hiyo katika nchi jirani, kama Comoros, umeiwezesha JKCI kufanya kambi za matibabu zinazookoa maisha nje ya mipaka kama ile waliofanya mwezi Novemba 2024. Ushirikiano huu muhimu ulitoa huduma muhimu za moyo kwa wagonjwa wengi na kuonesha umahiri wa matibabu wa Tanzania kimataifa.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Exim Bank, Stanley Kafu alielezea kuhusu mpango huu. “Exim Bank, tunajivunia sana kuwa mshirika wa muda mrefu katika safari ya JKCI ya kuokoa maisha ya Watanzania na hata nje ya mipaka. Uwekezaji wetu katika afya ya wafanyakazi wetu na umma wa Watanzania si jambo la muda mfupi; ni moja ya nguzo inayoonesha dhamira yetu. Uwepo wetu Comoros uliwezesha hivi karibuni tukashirikiana na JKCI kuandaa kambi za matibabu, kutoa huduma muhimu za moyo na kuonesha utaalam wa matibabu wa Tanzania.”
Zoezi hili, lililofanyika kwa wafanyakazi wa Makao Makuu ya Exim Bank, limeundwa kiutalaam kutoa huduma za afya kikamilifu. Linajumuisha elimu muhimu ya afya, vipimo vya kina vya shinikizo la damu, tathmini ya uzito na urefu (BMI), ushauri binafsi wa lishe, na vipimo muhimu vya moyo (ECHO) kwa washiriki wote. Lengo kuu la mpango huu makini ni kuhamasisha ustawi mahali pa kazi na kuwezesha ugunduzi wa mapema wa magonjwa yasiyoambukiza, hasa yale yanayohusiana na moyo, ambayo kwa bahati mbaya yanaongezeka miongoni mwa watu wazima duniani kote na Tanzania.
Kwa kuleta huduma hizi muhimu moja kwa moja kazini, Exim Bank na JKCI wanalenga kuwajengea wafanyakazi uwezo wa kuwa na maarifa na fursa za kuchukua hatua mapema, na hivyo kuwajenga kuwa na afya bora na tija zaidi.
Dkt. Tulizo Shem, akizungumza kwa niaba ya JKCI, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika afya ya umma. “Katika maadhimisho ya miaka 10 ya kuokoa maisha, tunatoa shukrani za dhati kwa msaada wa washirika wetu Exim Bank, mojawapo ya benki zinazoongoza nchini Tanzania. Ushirikiano wao umekuwa muhimu katika kuisaidia JKCI na taifa kufikia malengo yetu ya kitaifa ya afya. Mfano halisi ni jinsi walivyowezesha kambi yetu ya matibabu huko Comoros, ambayo haikutoa tu huduma za kuokoa maisha, bali pia iliwahimiza wagonjwa kutafuta matibabu ya hali ya juu hapa JKCI, na hivyo kukuza utalii wa matibabu kwa taifa.”
Ushirikiano huu kati ya Exim Bank Tanzania na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete unasimama kama ushahidi wenye nguvu wa athari chanya za ushirikiano wa kimkakati katika kukabiliana na changamoto muhimu za kiafya. Kwa kuweka kipaumbele katika afya ya wafanyakazi na afya ya jamii kwa ujumla, Exim Bank inaendelea kuongoza kwa mfano, ikisisitiza dhamira yake ya dhati ya kujenga Tanzania yenye afya bora na yenye nguvu zaidi.