Shirika la utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) wametumia maonesho ya Kilimo na Mifugo kuwakaribisha wazalishaji wa mkaa mbadala unaolenga kutunza na kulinda mazingira.
Hayo yameelezwa na mtaalam wa nishati kutoka TIRDO ndugu Paul Kimathi katika Viwanja vya Nane nane jijini Dodoma.
Ndugu Kimathi ameeleza kuwa uzalishaji wa mkaa mbadala kwa kutumia mabaki ya vyakula na mazao unalenga kusaidia kulinda mazingira kwa kutokata miti lakini pia kuongeza thamani ya mazao kwa wakulima.
“Mkaa huu unaouona umezalishwa kutokana na vifuu vya nazi, mapumba ya mpunga pamoja na magunzi” , unapotumia mabaki ya mazao ambayo huko nyuma yalikuwa yanatupwa au yanabaki kuchafua mazingira aliongeza Kimathi.
Ndugu Kimathi ameeleza kuwa wao kama TIRDO wamejikita katika kutoa elimu ya namna ya kuzalisha mkaa bora wenye manufaa kwa mazingira na watumiaji .
Katika Maonesho hayo TIRDO pia inatoa elimu juu ya matumizi bora ya nishati ya umeme na namna ya kupunguza gharama za umeme majumbani na viwandani.