

Mtoto wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Job Ndugai, Yustino Ndugai, ametoa salamu za shukrani kwa niaba ya familia mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mamia ya waombolezaji waliokusanyika kwenye Viwanja vya Bunge jijini Dodoma kwa ajili ya shughuli ya kumuaga.
Katika hotuba yake, Yustino alieleza kuwa familia inatoa shukrani za dhati kwa Rais Samia, Serikali, Bunge, viongozi wa dini, wananchi na wote walioshiriki katika kipindi chote cha msiba, akisema upendo na mshikamano uliodhihirishwa umeifariji familia katika wakati huu mgumu.
Shughuli ya kumuaga Hayati Ndugai imefanyika leo mjini Dodoma, kabla ya mwili wake kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Kongwa kwa mazishi yatakayofanyika kesho.