Na Mwandishi Wetu
Akizungumza katika mafunzo maalumu ya bloga yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ombi la Mtandao wa Bloga Tanzania (TBN), Dkt. Mkoko alisema blogu zina nafasi kubwa ya kuelimisha jamii, hivyo zinapaswa kutumika kwa uangalifu na weledi.
“Blog zina nguvu kubwa ya kusambaza taarifa kwa jamii, hivyo mnapaswa kuzitumia vizuri hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaingia kwenye uchaguzi mkuu,” alisema.
Alibainisha kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa Mwongozo wa Uandishi wa Habari za Uchaguzi ili kuhakikisha taarifa zinazochapishwa zinachangia kudumisha amani na utulivu nchini.

“Akili Bandia ikitumika vizuri inaongeza ufanisi wa mawasiliano, lakini ikitumiwa vibaya inaweza kuwa na madhara makubwa. Ni jukumu la watumiaji kuzingatia maadili na weledi,” alisisitiza.