Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo tarehe 12 Agosti, 2025 amekabidhi fomu ya uteuzi kwa mgombea wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano kutoka Chama cha Kijamii (CCK), David Daud Mwaijojele akiwa ameambatana na mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais kwa tiketi ya Chama hicho, Mhe. Masoud Ali Abdala katika Hafla hiyo ambayo imefanyika kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma.
………………….