NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus, akipata maelezo wakati akikagua mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” yaliyofanyika leo Agosti 12,2025 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus, amewataka vijana kote nchini kutumia maarifa, ujuzi na fursa zilizopo kwa bidii na nidhamu ili kujiletea maendeleo na kusaidia katika ustawi wa Taifa.
Bi. Zuhura ametoa wito huo leo, Agosti 12, 2025, jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.”
Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuwa bega kwa bega na vijana kwa kuhakikisha kuwa ndoto zao zinatimia kupitia mazingira rafiki ya kuwasaidia kujitegemea kiuchumi.
“Serikali imekuwa ikiimarisha mazingira ya kuwawezesha vijana kuanzisha na kuendesha shughuli za uzalishaji mali sambamba na kuchochea fursa za ajira kupitia mifuko na programu mbalimbali kama Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF), pamoja na asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri zinazotengwa kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu,” amesema Bi. Yunus
Bi. Yunus ameongeza kuwa vijana nchini wameendelea kunufaika na mikopo yenye masharti nafuu pamoja na mafunzo ya ujasiriamali ambayo yamewasaidia kuendesha shughuli zao kwa tija.
Hata hivyo amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha sera na mikakati mbalimbali ikiwemo Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana na Sera ya Ajira, ambazo zinalenga kukuza ujuzi wa vijana, kuongeza fursa za ajira na kuendeleza ubunifu unaowawezesha kushindana katika soko la ajira.
Aidha amewataka vijana wote nchini kushiriki katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025, kwa amani na utulivu ili kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
“Nitoe rai kwa vijana wote nchini kushiriki katika mchakato wote wa uchaguzi kwa amani na utulivu. Vijana mnatakiwa kuwa makini katika kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
“Kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, msingi mkuu wa maendeleo ni amani na usalama katika jamii zetu na vijana ndiyo kundi muhimu la kulinda na kudumisha amani ya Taifa letu,”amesema Bi. Yunus
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Suleiman Mvunye, amewataka vijana walioko vyuoni na waliomaliza elimu ya sekondari kuhakikisha wanajifunza stadi za maisha zitakazowawezesha kujipatia kipato halali na kujitegemea kiuchumi.
“Stadi za maisha kama ujasiriamali, ujuzi wa kiufundi na teknolojia ni nguzo muhimu kwa vijana kujikwamua kimaisha. Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya maendeleo ya vijana,” amesema Mvunye.
Naye Meneja wa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Joseph Manirakiza, ameeleza kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali katika kuwekeza kwa vijana kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus, akipata maelezo wakati akikagua mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” yaliyofanyika leo Agosti 12,2025 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus, akipata maelezo wakati akikagua mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” yaliyofanyika leo Agosti 12,2025 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus, akipata maelezo wakati akikagua mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” yaliyofanyika leo Agosti 12,2025 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus, akipata maelezo wakati akikagua mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” yaliyofanyika leo Agosti 12,2025 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus, akipata maelezo wakati akikagua mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” yaliyofanyika leo Agosti 12,2025 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus, akipata maelezo wakati akikagua mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” yaliyofanyika leo Agosti 12,2025 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana (LYED) Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Suleiman Mvunye,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” yaliyofanyika leo Agosti 12,2025 jijini Dodoma.
Meneja wa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Joseph Manirakiza,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” yaliyofanyika leo Agosti 12,2025 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus,(hayupo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” yaliyofanyika leo Agosti 12,2025 jijini Dodoma.

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa, ambayo mwaka huu yamebeba kaulimbiu: “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.” yaliyofanyika leo Agosti 12,2025 jijini Dodoma.