NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
MGOMBEA Udiwani wa Chama cha Mapinduzi kata ya Njia panda, John Meela (Chui) ameahidi endapo atachaguliwa kuwa Diwani atakahikisha kipaombele cha kwanza ni ujenzi wa barabara za ndani katika kata hiyo zinapitika kipindi chote.
Meela ambaye ni Mfanyabiashara katika mamlaka ya mji mdogo wa Himo ametoa kauli hiyo leo wakati alipochukua fomu ya kugombea Udiwani katika kata hiyo Ofisi ya Mtendaji wa Kata hiyo.
Amesema kuwa, moja ya vipaombele atakavyoanza navyo pindi akichaguliwa Oktoba 28 mwaka huu ni katika miundombinu ya barabara pamoja na Afya na Elimu.
Katika hatua nyingine Mgombea huyo alitumia nafasi hiyo kuwasihi na kuwaomba wanachama wa CCM katika kata ya Njia panda kuvunja makundi na kuwa wa moja kwani tayari Chama kimeshateuwa Mgombea hivyo jukumu la kila mwanachama ni kuhakikisha Chama kinashinda kwa kishindo.