LEVERKUSEN: MABINGWA wa zamani wa Bundesliga Bayer Leverkusen wametangaza kumsajili beki wa kimataifa wa Ufaransa Loic Bade kutoka Sevilla kwa mkataba wa miaka mitano.
Leverkusen, ambao wataanza msimu wao wa Bundesliga dhidi ya Hoffenheim Jumamosi, wameshuhudia zaidi ya wachezaji sita wakiondoka mwishoni mwa msimu huu, akiwemo beki wa kati Jonathan Tah, Florian Wirtz na mchezaji Granit Xhaka walioshinda nao mataji mawili ya ndani.
“Ndani ya Loic Bade tumesajili beki wa kati kijana na mwenye uzoefu mkubwa. Amezoea kucheza dhidi ya washambuliaji wa kiwango cha juu kabisa kwenye La Liga nchini Hispania,” -alisema mkurugenzi wa mchezo wa Leverkusen Simon Rolfes.
“Loic hana mchezo hata kidogo akiwa uwanjani anaweza kuusoma mechi haraka na kucheza jinsi mechi inavyomuhitaji, ni mtu kamili wa kuimarisha safu yetu ya ulinzi na kutufanya tuwe na kiwango cha juu cha ushindani msimu huu” – aliongeza.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 alianza soka lake Le Havre ya Ufaransa pia kwenda Nottingham Forest kwa mkopo kabla ya kukaa kwa misimu miwili na nusu nchini Hispania na Sevilla, ambayo alishinda nayo Europa League mwaka2023.
The post Bade ala tano Leverkusen first appeared on SpotiLEO.