Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ally Ussi, akifunga kongamano la Vijana, wilayani Ilemela, leo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ally Ussi, leo, akisistiza jambo wakati akifunga kongamano la Vijana, wilayani Ilemela.
Mchungaji Dk. Jacob Mutashi, leo, akitoa mada ya Uongozi na Uzalendo katika Kongamano la Vijana la kujadili fursa za Uchumi, wilayani Ilemela.
Ofisa Maendeleo ya Jamii, Manispaa ya Ilemela, Yusuf Okoko Omolo, akiwasilisha mada ya Fursa za kiuchumi, leo katika kongamano hilo.
Ofisa Uchaguzi Manispaa ya Ilemela, Shilinde Malyagili, akiwasilisha mada ya umuhimu wa vijana kushiriki uchaguzi, leo katika kongamano la vijana.
Mratibu wa Miradi wa Shirika la SOS, Kokutuna Kayungi, kwaslsha mada ya Stadi za Maisha, leo katikakongamano la vijana wilayani Ilemela.
Vijana wakwa katika kongamano la kujadl fursa za uchumi, uongozi, uzalendo,stadi za maisha, wilayani Ilemela, leo (Picha zote na Baltazar Mashaka)
……….
Na BALTAZAR MASHAKA, ILEMELA
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ally Ussi, amewataka vijana kote nchini, hususan wa Wilaya ya Ilemela, kuwa wazalendo, kutumia vyema fursa za kiuchumi ikiwemo mikopo ya asilimia 10 kutoka halmashauri, na kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na ustaarabu.
Ussi alitoa wito huo leo, alipofunga kongamano la vijana lililofanyika wilayani Ilemela, lililojadili mada mbalimbali ikiwemo fursa za uchumi, uongozi, uzalendo, afya ya uzazi, stadi za maisha, na malezi bora kwa vijana.
Akizungumza katika hafla hiyo, Ussi alisema lengo la makongamano hayo ni kuenzi na kuendeleza maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa kielelezo cha uongozi bora barani Afrika na duniani, wanaoleta heshima kwa wananchi wanaowatumikia, na hakuna kijana nchini hajashuhudia jitihada kubwa za maendeleo zinazofanywa na serikali yake.
“Kupitia kongamano hli, mmejifunza kuwa wazalendo,waadilifu, uongozi, malezi na makuzi, stadi za maisha,kushirik uchaguzi, na kujiunga na matumizi ya mfumo wa Nest, hivyo tunasisitiza vijana kuwa wabunifu na kujitokeza kuchangamkia fursa zinazotolewa Ilemela , kama mikopo ya fedha asilimia 10 ya mapato ya ndani imeanzishwa mahsusi kwa ajili yenu,” alisema.
Ussi alisema kuwa, ili kuepuka malalamiko ya kukosa mitaji, vijana baada ya kuunda vikundi watumie fursa za mikopo ya asilimia 10 kuibua fursa za kiuchumi.
“Vijana wazalendo nimewaona Ilemela, waliopatiwa fedha sh. milioni 50, wameweka heshima kubwa na kumheshimisha Rais Dk.Samia, yuko tayari kuona vijana wanakwenda kuibua fursa na kutumia fedha za mikopo kwa weledi,”alisema.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, aliwataka vijana kushiriki kwenye uchaguzi mkuu kwa amani na kupiga kura kwa wingi ili kulipa imani ya Rais Samia, kuonesha ukomavu wa kisiasa na kujiepusha na migogoro inayolenga kuvuruga amani.
“Mwaka huu ni wa uchaguzi kwa mujibu wa Ibara ya 42 kifungu cha pili (65) cha Katiba, vijana mkahamasishe wenzenu pamoja na familia ili wenye sifa wakashiriki kupiga kura na kutumiza haki yao ya kidemokrasia na kikatiba .
Kongamano hilo lilihusisha ushiriki wa taasisi binafsi na za serikali, ambapo vijana 1,123 walipatiwa mafunzo kuhusu uongozi, uzalendo, malezi na makuzi, stadi za maisha na mbinu za kujikwamua kiuchumi kupitia ujasiriamali.
Awali Mchungaji Dk.Jacob Mutashi akiwaslisha mada ya uongozi na uzalendo, alisema wazazi wanapaswa kuwaeleza vijana historia ya taifa letu, mazuri ya maendeleo ili waelewe badala ya kuponda kila kitu, huku akiwataka vijana kuiga mfano wa Mwalimu Julius K.Nyerere , kwa uzalendo wa kuipenda nchi yake aliacha Ualimu ili kupambana na wakoloni.
Naye Jabir Bane wa PPRA alisema asilmia 30 ya bajeti ya serikali hupelekwa katika taasisi kwa ajili ya wananchi, vijana wamepewa upendeleo wa asilimia 10, ili wanufaike kwa mkopo huo wakajisajili kwenye vikundi na katika mfumo wa Nest pamoja na halmashauri, wakionesha shughuli wanazofanya.
Aidha, kongamano hilo liliambatana na wito kwa vijana kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani ya nchi, kushiriki shughuli za maendeleo na kuwa mawakala wa mabadiliko chanya katika jamii.