Na John Mapepele
Mgombea wa Nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Rufiji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)na MNEC kupitia Mkoa wa Pwani, Ndugu Mohamed Omary Mchengerwa amewaongoza maelefu ya wanaCCM wa Mkoa wa Pwani kuhudhuria uzinduzi wakihistoria wa kampeni ya mgombea wa urais kwa CCM Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Uzinduzi huu unafanyika leo katika viwanja vya kawe jijini Dar es Salaam huku maelfu ya wananchi na wanaCCM kutoka katika mikoa mbalimbali nchini wakifurika kushuhudia uzinduzi huu.
Aidha, uzinduzi huu imepambwa na wasanii mbalimbali ambao wameburidisha umati wa maelfu ya wananchi waliohudhuria.
Tayari Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imempitisha Mhe. Mchengerwa kugombea Ubunge jimbo la Rufiji baada ya kurejesha Fomu za ubunge Utete wilayani Rufiji.
Mhe. Mchengerwa maarufu kwa jina la Mchengerwa Mtu Kazi ( MMK) anaingia kwenye kinyang’anyiro cha kutetea kiti chake cha ubunge baada ya kuliongoza jimbo hilo kwa mafanikio makubwa.
Miongoni mwa mapinduzi makubwa aliyoyafikia katika jimbo hilo kwa kushirikiana na wananchi wa Rufiji ni pamoja na mafanikio kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara na taa za barabara, madaraja, madarasa na maji.
Pia katika sekta ya Afya kumekuwa na ongezeko la zahanati, vituo vya afya na hospitali.
Katika zoezi la kura za kusaka mgombea ubunge wa CCM kwa jimbo la Rufiji mwaka huu ambao ulikuwa na wagombea wanne wa nafasi hiyo Mhe. Mchengerwa aliweza kushinda kwa zaidi ya asilimia 99 ya kura zote zilizopigwa.