NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Ally Salumu Hapi, amezindua kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Segerea,jijini Dar es Salaam na kuwataka wananchi kuchagua wagombea makini wa CCM.
Wagombea hao ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hasan, mgombea ubunge wa jimbo hilo,Bonnah Kamoli na wagombea udiwani.
Hapi amewataka wananchi katika Jimbo la Segerea, kuhakikisha katika uchaguzi huu hawafanyi makosa kwa kuchagua wagombea wa upinzani ambao vyama vyao havina sera wala Ilani.
“Mchagueni ni Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, mgombea ubunge wa Jimbo hili Bonnah Kamoli na madiwani wote wa CCM wawaletee maendeleo,”ameeleza.
Amesema wananchi wa Segerea ni lazima waamini ucchaguzi siyo tukio bali ni hatma yao ya miaka mitaono.”Tuchague viongozi wenye sifa wanaoweza kumfikia Rais Dk. Samia na kupanga maendeleo,”amebainisha Hapi.
Chagueni viongozi wenye sifa wanaoweza kuwaletea maendeleo.
Achaneni na vyama vya ubwabwa, CCM ni chama chenye ilani iliyopangwa, chama chenye mikakati iliyo pangika,” amebainisha Hapi.
Amesema kwa wanachama wa CCM katiba imwelekeza uamimifu kwa Chama hivyo uaminifu huo ni pamoja na kumchagua Rais DK. Samia, madiwani na wabunge wa CCM.”Segerea mna bahati, mnashule za ghorofa. Ni mapenzi ya Rais dk. Samia .
Haina maeneo ya kujenga shule ila kutokana na mapenzi ya Rais Dk. Samia na upendo wa mbunge wenu Bonnah, mliingiziwa mabilioni na shule imejengwa,” amebainisha Hapi
Hapi amedai Oktoba 29 mwaka huu CCM inakwenda kuzitafuta kura nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa na kitanda kwa kitanda.
” Niwaombe wananchi wa Segerea chahueni watu wanao jua kuzungumza na serikali. Chagueni Chama chenye sera inayo tekelezeka.Chagueni Kiongozi mwenye ‘connection,”amesema.Pia huduma za kuto maiti hospitali itakuwa bure na ataanza majaribio ya bima ya afya iliyoboreshwa Kwa wazee na watoto.
Ameongeza: ” Mchagueni Bonnah kuwa Mbunge wa Segerea Kwa sababu ana connection na CCM Chama chenye Ilani inayo tekelezeka. Ana connection na Rais Dk. Samia,”
Kwa upande wake mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah, aliwaomba wananchi kuendelea kumwamini yeye na Rais Dk.Samia, kwa kuwapa kura za kishindo Oktoba 29.
“Ninamshukuru Rais Dk. Samia, Segerea inapiga hatua kubwa Kwa maendeleo. Nakiri kulikuwa na changamoto kubwa ya ubovu WA barabara na masaraja. Tunaendelea kukabiliana nazo.,” amesema Bonnah.
Amesema, changamoto hiyo ya barabara ilitoka na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutokuwa na Mradi wa Uboreshji Miundombinu ya jiji hilo (DMDP).
” Sasa barabara zetu zimeingizwa katika mradi huo. Wakamdarasi wako kazini. Madaraja na baadhi ya barabara zinakengwa na tutaendelea kukabiliana na changamoto hii,” amese Bonnah.
Ametaja changamoto nyingine iliyopatiwa ufumbuzi kuwa na uhaba wa maji na mikopo ya asilimia 10 ya wajasiriamali inayoonekana na mapato ya ndani ya Halmashauri kuto kutolewa Kwa wakati.
Alisema Rais Dk, Samia, alikwisha ruhusu mikopo hiyo kutolewa hivyo kuwatoa wasiwasi wananchi wa jmbo hilo.