
Wananchi na wakereketwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza kwa wingi kuonesha imani yao kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kampeni zinazoendelea kote nchini.
Leo, Septemba 3, 2025, Dkt. Samia anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa kampeni katika Mkoa wa Songwe, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Ziara hiyo inatarajiwa kukusanya maelfu ya wananchi na wafuasi wa chama hicho, huku viongozi mbalimbali wa kitaifa na kikanda wakihamasisha mshikamano na mshikikano wa kisiasa kwa ajili ya ushindi wa CCM katika ngazi zote.