Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano ya Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja akiwataka wajumbe wa Kamati hiyo kushirikiana na Kitengo hicho katika kufanikisha utoaji wa taarifa kwa umma, wakati wa Kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.
Afisa Habari wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Joseph Mahumi, akitoa mada kuhusu mitandao ya kijamii inayomilikiwa na Wizara wakati wa Kikao kazi na Kamati ya Mawasiliano ya Wizara hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka Idara na Vitengo vya Wizara, jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano ya Wizara ya Fedha ambaye pia ni Afisa Mwandamizi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu, Bw. Gema Mwakyusa, akieleza kuhusu upatikanaji wa taarifa, wakati wa kikao kazi cha Kamati hiyo, jijini Dodoma. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo, Bw. Jeremiah Kyellu.
Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano Wizara ya Fedha, kutoka Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Bw. Hamisi Mvungi akieleza umuhimu wa kushirikiana na Kitengo cha Mawasiliano ili kuwa na taarifa sahihi na zinazotolewa kwa wakati, wakati wa Kikao kazi cha Kamati hiyo, jijni Dodoma. Kushoto ni Mjumbe kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Yambi Kinyaki.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Wizaravya Fedha, ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja akiongoza Kikao kazi cha Kamati hiyo kuhusu kufanikisha utoaji wa taarifa kwa umma, wakati wa Kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu Fungu 50 Wizara ya Fedha, Bw. Jeremiah Kyellu, akieleza jambo wakati wa Kikao kazi cha Kamati hiyo, jijini Dodoma, kushoto ni Afisa Habari wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bi. Farida Ramadhani.
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao kazi cha Kamati ya Mawasiliano Wizara ya Fedha, wakifuatilia mada zilizolenga kuongeza ufanisi katika utoaji taarifa kwa umma kuhusu majukumu, program na sera za Wizara, kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, akifuatilia taarifa za kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika jijini Dodoma, kushoto ni Afisa Mkuu wa Kitengo hicho, Bi. Scola Malinga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja (Katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano Wizara ya Fedha, baada ya kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Dodoma)
…………
Na. Peter Haule, WF, Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja amewataka wajumbe wa Kamati hiyo kuwa sehemu ya kufanikisha utoaji taarifa sahihi na kwa wakati kwa umma ili kutimiza haki ya wananchi kupata taarifa.
Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma wakati wa Kikao kazi cha Kamati hiyo kinachohusisha wajumbe kutoka Idara na Vitengo vya Wizara kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa matumizi ya umma.
Bw. Mwaipaja alisema kuwa Wizara ina jukumu la kutoa taarifa kwa umma kuhusu sera, program, mipango na matukio ya Wizara ili kuuwezesha umma kuwa na uelewa kuhusu majukumu ya Wizara na mambo mengine.
“Nitoe rai kwa wajumbe wa Kamati hii kuhakikisha mnatoa ushirikiano kwa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa kuainisha kalenda za matukio muhimu kwa umma ili kitengo kiweze kuzifanyia kazi”, alisema Bw. Mwaipaja.
Alisema taarifa zinazopatikana hutumika kuandaa majarida ya Wizara lakini pia kuwezesha kutoa taarifa kupitia Tovuti ya Wizara, Instagram, Whatsap, Tweeter, Linkidin Hazina Tv na vyombo vingine vya Habari kama runinga na magazeti.
Alisema kuwa tayari Wizara imetoa Jarida la Hazina Yetu Toleo la Nne ambalo limesheheni taarifa muhimu kwa umma na inaendelea na kuandaa Toleo la Tano ambalo linategemea taarifa zilizopo katika Idara na Vitengo vya Wizara.
Alisema kuwa kupitia chaneli mbalimbali za mawasiliano ambazo Wizara hutumia kuwasilisha Majarida hayo, kuna wadau ambao wanahitaji kuendelea kutoa taarifa kwa kuwa zinaandaliwa kwa lugha nyepesi yenye kueleweka kwa watu mbalimbali.
Aidha, amewataka wajumbe hao kuendelea kuhamasisha wadau wa ndani na nje kufuatilia taarifa zinazotolewa na Wizara kwa manufaa yao katika kuongeza maarifa na matumizi mengine ya tafiti za kitaaluma.