Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt. Asha – Rose Migiro Leo tarehe 12 Septemba,2025 amefanya Kikao cha Sekretarieti Ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, Kwa ajili ya kuzungumza Maendeleo ya Maandalizi ya Uzinduzi wa Kampeni za CCM, 2025 Kwa Upande wa Zanzibar.
Katibu Mkuu amepokea Taarifa za Utekelezaji wa Kamati zinazo Kamilisha Maandalizi ya Mkutano huo, Mambo yaliojadiliwa na kupatiwa majawabu Kwa ufanisi ni Usafirishaji, Hali ya Uwanja, Majukwaa na Mapambo.Pamoja na kupokea taarifa za Vyombo vya Habari, Mawasiliano na Burundani. Katibu Mkuu pia ametaka kufahamu suala la huduma muhimu za Afya, na Ulinzi na Usalama upo.
Na katika kikao hicho imetolewa Ratiba ya Mkutano wa Kampeni za CCM wa tarehe 13/9/2025