Leo Septemba 15, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro, ili kuanza rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani humo.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika eneo la Nyabibuye, Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma baada ya kuhitimisha Mbio zake katika mkoani Kagera.