LONDON: BAADA ya kukamilika kwa Raundi ya tatu ya kombe la Carabao usiku wa Jumatano. Droo ya raundi ya nne au 16 bora ya kombe hilo imewekwa hadharani ambapo vigogo mbalimbali wa soka la England wamefahamu wapinzani wao katika hatua hiyo.
Katika droo hiyo mabingwa watetezi Newcastle United wataanza kampeni ya kutetea kombe lao nyumbani kwa Tottenham Hotspur katika moja ya mechi zitakazokuwa na mvuto wa aina yake huku Arsenal dhidi Brighton, Liverpool dhidi ya Crystal Palace na Wolverhampton dhidi ya Chelsea ikiwa ni michezo yenye sura ya EPL ndani ya raundi hiyo.
Wrexham, timu maarufu ya daraja la pili inayomilikiwa kwa ubia na mwigizaji wa filamu ya “Deadpool” Ryan Reynolds, itacheza na mpinzani wake wa Wales Cardiff City nyumbani.
Manchester city watasafiri hadi Swansea kuvaana na wababe wa zamani wa EPL Swansea City waliofuzu kwa raundi hiyo ya nne sambaba na Wrexham timu pekee kutoka visiwa vya Wales.
Droo kamili ni kama ifuatavyo
Grimsby Town v Brentford
Swansea City v Manchester City
Newcastle United v Tottenham Hotspur
Wrexham v Cardiff City
Liverpool v Crystal Palace
Wolverhampton Wanderers v Chelsea
Wycombe Wanderers v Fulham
Michezo hii inatarajia kuanza kutimua vumbi katika wiki ya Oktoba 27.
The post Moto kuwaka raundi ya nne Carabao Cup first appeared on SpotiLEO.