Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Huduma za Shirika Ngorongoro Bw. Aidan Makalla (kulia) akiwa ameambatana na Abdiel Laizer Afisa Utalii Mkuu Msaidizi amekutana na Mawakala mbalimbali wa utalii kunadi Fursa za Utalii na uwekezaji zilizopo Ngorongoro katika Maonesho ya “My Tanzania Roadshow 2025 Europe” yayofanyika katika miji ya Stuttgat – Ujerumani, Salzbug- Austria; Ljubljana – Slovania and mji wa Milan Nchini Italia kuanzia tarehe 22- 27 Septemba, 2025.
Maonesho hayo ambayo huandaliwa na Kampuni ya KILIFAIR ni moja ya majukwaa ya kipekee yanayolenga kutangaza vivutio vya utalii na kuitangaza Tanzania kama kitovu cha Utalii ktika soko la Ulaya ambapo zaidi ya Kampuni 80 kutoka Tanzania na Ujerumani zinashiriki maonesho hayo.