Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Haki za Binadamu na Utawala Bora sehemu ya Utawala Bora ya Tume za Haki za Binadamu na Utawala Bora THBUB, Bw. Mbwana Mussa Mbwana akizungumza na wafanyakazi wa tume hiyo katika ofisi zake za Zanzibar zilizopo Mombasa Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 26 Septemba, 2025.
Kaimu Afisa Mfawi wa Tume za Haki za Binadamu na Utawala Bora THBUB, Zanzibar Bw. Wilfred Msagati (aliyesimama) akitoa shukurani baada ya kikao na wafanyakazi wa tume hiyo katika ofisi zao zilizopo Mombasa Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 26 Septemba, 2025.
……
MKURUGENZI Msaidizi kutoka Idara ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) sehemu ya Utawala Bora Bw. Mbwana Mussa Mbwana akizungumza na watumishi wa Tume hiyo Ofisi ya Zanzibar, kwenye ukumbi wa Ofisi hiyo, Mombasa Wilaya ya Magharibi B, tarehe 26 Septemba, 2025.
Katika nasaha zake, amewahimiza ushirikiano baina yao katika utekelezaji wa kazi za tume hiyo.
Aidha, amewakumbusha zaidi watumishi hao kujali na kuzingatia muda wa kuwasili na kuondoka kazini sambamba na kudumisha uadilifu wakiwa kwenye majukumu yao ya kila siku.
Akizungumzia suala la mavazi Mkurugenzi huyo aliwasisitiza watumishi hao kuendelea kutii Sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma kwa kuzingatia mavazi yaliyoainishwa na utumishi wa umma.
Kwa upande wake Kaimu Mfawidhi THBUB ofisi ya Zanzibar ambaye pia ni Afisa Sheria bw. Wilfred Msagati, amepongeza na ujio wa kiongozi huyuo kwenye ofisi za Zanzibar na kuahidi kuzifanyia kazi nasaha za kiongozi hiyo kwa kumuhakikisha uweledi wa tume kutokana na kuongezeka kwa nguvu kazi.
Naye, Mwandishi mwendesha ofisi, bi. Salha Hamza kwa niaba ya watumishi wa Ofisi hiyo walimshukuru Mkurugenzi Mussa kwa nasaha na ushirikiano alioutoa kwa ofisi hiyo. Bw. Mussa alikuwepo ofisi za THBUB Zanazibar kwa ziara ya kikazi.