Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa, wameungana na Maaskofu, Mapadri, Viongozi wa Kanisa Katoliki na waumini kushiriki Misa Takatifu ya mazishi ya Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, Balozi wa Baba Mtakatifu.
Misa hiyo Takatifu imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Kardinali Protase Rugambwa, katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo la Bukoba, mkoani Kagera, leo tarehe 29 Septemba 2025.
Viongozi mbalimbali na wanafamilia walishiriki Misa hiyo, akiwemo Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Wolgang Pisa; Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Mkuu Angelo Acattino; Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Mhashamu Jovitus Mwijage; pamoja na Mapadri, Watawa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, na waamini kutoka ndani na nje ya mkoa wa Kagera.