NA DENIS MLOWE , IRINGA
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya CCM, Fadhili Ngajilo ameahidi wananchi wa kata ya Nduli kuwa akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha kuwa eneo la Mapanda kutajengwa viwanda vidogo vidogo ili kuzalisha ajira kwa vijana.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM wakiwemo Mratibu wa Kampeni wa Jimbo hilo, Salvatory Ngerela, na aliyekuwa meya wa manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada, Mgombea ubunge Fadhil Ngajilo alisema kuwa lengo kuanzishwa viwanda hivyo ni kuzalisha bidhaa na kuchochea ajira kwa jamii hususani vijana na kuongeza mzunguko wa fedha katika kata ya Nduli.
Ngajilo alisema kuwa kufanikisha hayo katika kata ya Nduli wakumbuke kuwa maendeleo hayaji bila ushirikiano wa karibu kati ya viongozi na wananchi na kuwataka kumpa ushirikiano kuwaletea maendeleo yao.
Akizungumzia kuhusu changamoto ambazo haziitaji kupelekwa hata bungeni kama maji na umeme alisema kuwa kila kitu kipo sawa kinachohitajika ni watu kupelekewa umeme na maji kwani miundo mbinu ipo tayari.
“Nduli tutashughulika na kila changamoto zote ambazo mgombea udiwani ameniagiza hivyo kura zenu ndio ukombozi wenU suala la maji,umeme ni jambo ambalo tunalimudu kwani changamoto kubwa ni umeme kuwafikia watu kwani miundo mbinu ipo” Alisema.
Aliongeza kuwa kazi yangu ni kuhakikisha mnapata maendeleo na Nduli changamoto ya mawasiliano ya simu ni ngumu sana hivyo hilo tutashughulika nalo hapa hapa sio kutupeleka bungeni kwani nikiwa mbunge mambo makubwa ndio anatakiwa kupelekewa rais kama kuongezea nguvu kwenye ujenzi wa barabara.
Alisema kuwa kata ya Nduli mnahitaji barabara nzuri iwe za rami hadi Changalawe hivyo endapo akichaguliwa kuwa mbunge atahakikisha zinajengwa ili ziweze kupitika nyakati zote.
Aidha aliongeza kuwa endapo atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha wakazi wa kata ya Nduli atashughulikia changamoto ya wakulima kuhusu mbolea kuwafikia kwa wakati na yenye ubora.
Aidha atahakikisha Kata ya Nduli linajengwavl Soko ambalo litawasaidia wakazi wa kata hiyo.
Ngajilo alibainisha kuwa endapo atakuwa Mbunge atapigania mkoa wa Iringa kuwa jiji hivyo ni vita kubwa ambayo inahitaji kuwa kamili katika Miundo mbinu na kuendelea kutatua changamoto zilizopo.
Vilevile alisema kuwa Nduli ni kata ya kimkakati kuwepo kwa kiwanja cha ndege ni faida kubwa atahakikisha kuwa uwanja unabadilishe maisha watu wa Nduli hivyo tutakuwa na vikao ili kuona tunabadilisha vipi maisha kupitia uwanja wa ndege.
Aidha alisema kuwa atahakikisha wananchi wa Kata hiyo wanarasimisha ardhi kuweza kufanya kazi zenu kwa amani na nyumba zenu ziwe rasmi hivyo tutafanyia kazi kwa kushirikiana na diwani.
Ngajilo aliwataka wananchi wa Iringa Mjini kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa Rais, wabunge na madiwani wa CCM, akisema kura nyingi ndizo zitakazoongeza hamasa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake mgombea udiwani wa Kata ya Nduli, Bashir Mtove alisema kuwa ataendelea kuboresha barabara za vumbi ili ziweze kupitika muda wote.
Alisema kuwa wakimchagua tena atahakikisha anapambana Zahanati ya Nduli ipandishwe iwe kituo cha afya kutokana na mahitaji zaidi kwa wananchi na kuomba kwamba Kata ya nduli kuongezewa shule ya sekondari eneo la Kigonzile.