Mwezeshaji kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Seif Khamis Moh’d akitoa elimu ya Mfuko huo kwa Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora THBUB ofisi ya Zanzibar, kupitia Semina ya wanachama wa mfuko huo, hapo ofisi za THBUB Mombasa, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Oktoba, 2025.
Maofisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora THBUB ofisi ya Zanzibar, wakimsikiliza Bw.Seif Khamis Moh’d (hayupo pichani) wakati wakipatiwa semina ya wanachama wa mfuko huo katika ofisi za THBUB zilizopo Mombasa, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, jana.
…………..
KAMISHNA wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Ofisi ya Zanzibar, Mhe. Khatibu M. Mwinyichande amewahimiza watumishi wa tume hiyo kujijengea ustawi bora na mazingira mazuri endapo watastaafu.
Mhe. Mwinyichande alitoa nasaha hizo jana ofisini kwao Mombasa Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi kupitia semina ya wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) waliopewa watumishi wa tume hiyo.
Aidha aliwasihi watumishi hao kujiunga na mfuko huo kwani ni mzuri na una faida kwao na kwa familia zao, akilisifia ‘fao la kifo’ ambalo litamnufaisha mtumishi wa mfuko huo hata baada ya kuondoka duniani.
Naye, Katibu Msaidizi THBUB, Bw. Juma Msafiri Karibona aliishukuru PSSSF kwa ushirikiano wanaoutoa kwa watumishi wa umma sambamba na kuwaomba kuwafikia watumishi wa THBUB kisiwani Pemba.
Mapema, akichambua mada ya ‘fao la kifo’, mbali na mafao mengine aliyoyajadili kwenye semina hiyo, yakiwemo mafao ya uzazi, uzee, ulemavu, kukosa ajira, ugonjwa na fao la wategemezi, Afisa huduma kwa wateja wa mfuko wa PSSSF, Ndg. Marry Malilo amesema, Mtumishi wa umma akiwa mwanachama wa mfuko huo endapo atafariki watamchangia marehemu shilingi laki tano kwenye mazishi yake, mbali na kutoa mafao mengine ya urithi kwa warithi halali wa marehemu pia mfuko utaendelea kuwalipa mpencheni ‘Mjane’ au ‘Mgane’ wa marehemu pamoja na watoto wa marehemu walio chini ya umri wa miaka 18 kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo na watalipwa kima cha mshahara aliokua akiupokea marehemu.
Kwa uapande wake Mwezeshaji wa Mfuko huo, Bw. Seif Khamis Moh’d wakati akitoa elimu ya Mfuko huo kwa Watumishi wa THBUB kupitia Semina ya wanachama wa mfuko huo, aliwashauri kujipanga mapema kimaendeleo kabla ya kusubiri kustaafu.
Aliwahimiza watumishi hao kupitia mada ya ‘kustaafu’ aliwasihi kujiandaa mapema kwa kijiwekea akiba mapema ili kujijengea mazingira nazuri watapo staafu.
Aidha, aliwashauri watumishi hao kuanza mapema kujiekeza kwenye uchumi kwa kujiwekeza mapema kabla ya kustaafu kwao.
Hata, hivyo aliwasihi watumishi hao kujiepusha na maisha ya anasa na ya fahari kubwa kwa kipindi chote cha utumishi wao ili wapate nafasi ya kujiwekea akiba endapo watafikia mwisho wa utumishi wao (kustaafu).
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ulianzishwa mwaka 2018.