
Staa wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani, Sean ‘Diddy’ Combs amehukumiwa kwenda jela miezi 50 (sawa na miaka 4 na miezi 2) baada ya kukutwa na hatia katika makosa mawili yaliyokuwa yakimkabili yanayohusiana na usafirishaji wa watu kwa ajili ya ukahaba.
Diddy ambaye amekuwa gerezani jijini Brooklyn, New York tangu alipokamatwa Septemba, 2024, amekutwa na hatia ya kuwasafirisha wapenzi wake wawili wa zamani na kuwalazimisha kushiriki ngono na wanaume waliolipwa kwenye sherehe zake binafsi za Freak Offs.
Kesi dhidi yake iliendeshwa kwa muda wa miezi miwili katika mahakama ya Manhattan msimu wa kiangazi.
WATOTO WATATU wa FAMILIA MOJA WAFARIKI DUNIA NYUMBA IKITEKETEA kwa MOTO KIBAHA POLISI WATHIBITISHA..