
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesimamisha kwa muda mchezaji wa klabu ya Yanga Queens, Princess Jeanine Mukandiyisenga, raia wa Rwanda, kupisha uchunguzi wa kina kuhusu jinsia yake.
Hatua hii imekuja baada ya sintofahamu kuibuka mitandaoni na katika baadhi ya duru za michezo, ambapo mashabiki na wadau wameanza kuhoji hali halisi ya jinsia ya mchezaji huyo, ambaye amekuwa akionesha kiwango cha juu mno katika michezo ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya TFF, uchunguzi huo unalenga kuthibitisha ukweli bila upendeleo, kwa mujibu wa kanuni za shirikisho hilo na taratibu za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuhusu wachezaji wa kike.
Kwa sasa, Mukandiyisenga atabaki nje ya kikosi cha Yanga Queens hadi uchunguzi utakapokamilika na matokeo rasmi kutolewa.
TFF imewataka mashabiki na wadau wote wa soka kuwa watulivu na kuepuka kutoa maoni ya kudhalilisha au ya kibaguzi, ikisisitiza kuwa mchakato huu ni wa kawaida na wa kisheria katika michezo ya kimataifa.
MASHEKH ARUSHA WALIOHUSISHWA na POLEPOLE WAFUNGUKA – “‘TULIMUONYA” – WATUMA UJUMBE KUELEKEA UCHAGUZI