

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limemteua Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Soka la Ufukweni ya FIFA kwa kipindi cha miaka minne, hadi mwaka 2029.
Uteuzi huu unamweka Karia katika historia kama Mtanzania wa kwanza kushika nafasi ya juu ndani ya uongozi wa FIFA, hatua inayodhihirisha hadhi na heshima inayoongezeka kwa soka la Tanzania katika ngazi ya kimataifa.
Aidha, Karia ni miongoni mwa Marais watano pekee wa mashirikisho ya soka barani Afrika walioteuliwa na FIFA kushika nafasi mbalimbali katika kamati zake kuu, jambo linaloonesha imani kubwa ya shirikisho hilo kwa viongozi wa Afrika.
KESI YA LISSU BADO KISIKI/SIKU YA PILI BILA TAARIFA ZA POLEPOLE-MAMA AANGUA KILIO/ACT KIKAONI