
Jeshi la Polisi nchini limetoa tamko rasmi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ambapo wananchi wamehakikishiwa usalama na kwamba hakuna tishio lolote la kiusalama litakalozuia watu kupiga kura.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime, amesema mtu yeyote atakayethubutu kuvunja sheria, asilaumu kwa hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yake.







