DODOMA: Msanii wa vichekesho Emmanuel Mathias, maarufu kama Mc Pilipili, ambaye amefariki dunia jana Novemba 16, 2025 , anatarajiwa kuagwa na kuzikwa Alhamisi, Novemba 20, 2025, nyumbani kwao Swaswa, mkoani Dodoma.
Taarifa hizo zimetolewa na rafiki yake wa karibu, Godfrey Lughalabamu ‘Gara B’, ambaye amethibitisha kuwa msiba upo nyumbani kwa familia ya Mc Pilipili eneo la Swaswa, ambako maandalizi ya mazishi yanaendelea.
Kwa mujibu wa Gara B, marehemu atapumzishwa rasmi siku ya Alhamisi, ambapo ndugu, jamaa na marafiki wanatarajiwa kuhudhuria ili kutoa heshima za mwisho. “Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe,” amesema.
Source SpotiLEO.





