NAIBU Waziri wa Uchukuzi,David Kihenzile akizungumza kwenye mkutano huo jijini Arusha.

………
Na Happy Lazaro, Arusha
NAIBU Waziri wa Uchukuzi,David Kihenzile amewataka watendaji wakuu wa sekta hiyo na wadau binafsi kutimiza wajibu kwa weledi na uzalendo ili kuendana na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuifanya sekata hiyo kuwa muhimili mkubwa wa pato la Taifa na kichocheo cha mabadiliko ya kiuchumi kuelekea Dira ya Taifa ya 2025-2050.
Akizungumza Jijini Arusha wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 18 wa Tathimini wa Sekta ya Uchukuzi 2024/25 na kiupanga mpango kazi wa mwaka ujao,Kihenzile alisema serikali ya awamu ya sita itaendelea kutenga fedha kwa ajili miradi ya maendeleo ikiwemo reli,bandari,viwanja vya ndege,usafiri wan chi kavu na majini pamoja na mifumo ya kisasa ya usafirishaaji ili kuhakikisha sekata hiyo inafanya kazi kw aufanisi na kuchangia kwa kiwango kikubwa Uchumi wan chi.
Ame
ema serikali imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 88 kupitia sekta ya reli, na tayari serikali imesaini mkataba wa kuunganisha reli ya SGR kati ya Tanzania na Burundi, sambamba na mipango ya kuendelea kuboresha reli ya meter gauge pamoja na mifumo mingine ya uchukuzi lengo ni kutaka sekta hiyo kuwa mkombozi katika kuinua Uchumi wa nchi.
Kihenzile amesema mkutano huo unatoa fursa muhimu ya kujadili kwa kina namna ya kuimarisha reli ya TAZARA, huku serikali ikiendelea kutekeleza maboresho katika bandari na sekta ya usafiri wa majini, ikiwa ni sehemu ya mkakati mpana wa kuboresha miundombinu ya Taifa.
‘’Niwaombe watendaji wakuu kila mmoja akajipange katika kuboresha sekta anayoiongoza ili mwakani tukikutana malengo yawe yamefikiwa na kuzidi na hataki kusikia visingizio wakati Rais ameshatoa fedha hii haikubaliki’’amesema Kihenzile
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,profesa Godius Kahyarara, amesema serikali inaendelea kurasimisha sekta ya bodaboda kutokana na mchango wake mkubwa katika ajira kwa vijana, ambapo sekta hiyo inaajiri kati ya asilimia 8 hadi 10 ya vijana nchini.
Kyaharara amesema kwa sasa sekta ya uchukuzi inachangia dola zaidi ya shilingi milioni 2.6 katika mapato ya serikali, hali inayodhihirisha nafasi yake kama nguzo muhimu ya ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Katika mkutano huo, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imepongezwa kwa matumizi ya mifumo ya kisasa na usimamizi wa haki katika utoaji wa fursa ndani ya sekta ya uchukuzi.
Kaimu mkurugenzi ufuatiliaji na tathmini wizara ya uchukuzi Devota Gabriel amesema huu ni mkutano wa kisera katika kufiatilia na kutathmini mafanikio ya sekta ya uchukuzi nchini na kupanga mkakati wa utendaji wa kipindi kijacho lengo likiwa moja tu sekata hiyo kufanya vema katika Uchumi wa nchi.
Amesema kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu wa siku tatu ambao utafungwa na Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa kesh oni “Mifumo Jumuishi ya Usafirishaji kama Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi kuelekea Dira ya Taifa ya 2050.”






