NA DENIS MLOWE – IRINGA
KATIKA Mkoa Iringa, kata ya Isakalilo kuna shule ambayo kwa sasa ni habari ya mjini ya Good Victory English Medium School imeendelea kujidhihirisha kama moja ya taasisi bora zaidi za malezi na elimu nchini, ikiwa na rekodi ya ufaulu wa hali ya juu na mfumo wa kipekee wa kumlea mtoto katika misingi ya kitaaluma, kimaadili na kiufundi.
Shule hii, iliyosajiliwa rasmi mwaka 2018 chini ya namba EM 17702, inatoa elimu ya awali na msingi kwa kutumia lugha ya Kiingereza, ikiwa na mazingira rafiki, salama na yenye miundombinu ya kisasa ikiwemo mfumo wa kamera darasani, mabwenini na maeneo ya wazi ili kuhakikisha usalama na uangalizi wa watoto muda wote.
Ufaulu wa Kipekee Kitaifa
Good Victory English Medium School imeweka historia mwaka 2024, baada ya wanafunzi wa darasa la saba kushika nafasi ya kwanza Tanzania Bara na Visiwani, wakipata asilimia 99.99 katika ufaulu wa mtihani wa taifa.
Kadhalika, tangu mwaka 2019 shule imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya darasa la nne na saba, na kufikia hadhi ya kuwa miongoni mwa shule zinazotajwa kila mwaka kwa matokeo bora mkoani Iringa na kitaifa.
Mwalimu Amos Koneri Kimolimoli Mwalimu wa Taaluma shule ni hapo anabainisha kuwa mbinu mseto za kufundishia, ikiwemo ushirikishwaji, matumizi ya teaching aids, matumizi ya picha na mbinu bunifu, zimechangia kuwafikia wanafunzi wote kulingana na tofauti zao za uelewa.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Sabatho Joashua anasema kuwa Mkazo Mkubwa Katika Malezi na Nidhamu kwa mujibu wa uongozi, misingi ya mafanikio ya shule imejikita katika kumjua mtoto mmoja mmoja, tabia, uwezo na changamoto zake.
Anaongeza kuwa Shule huwashirikisha wazazi katika mchakato wa malezi na elimu ili kuhakikisha mtoto anakua kwa mwelekeo sahihi.
Uongozi unaamini kuwa, “Mtoto mwenye hofu ya Mungu lazima awe na nidhamu, na nidhamu njema humsaidia kufanya vizuri kitaaluma.”
Kwa msingi huo, shule inaendesha vipindi vya dini mara moja kwa wiki, huku wanafunzi wakipelekwa kanisani au msikitini kulingana na imani yao. Watoto wa bweni hupelekwa kwa usafiri maalum wa shule siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.
Kuandaa Mtoto wa Karne ya 21 Kompyuta, Teknolojia na Stadi za Maisha
Good Victory English Medium School inatambua kuwa dunia ya leo inaongozwa na teknolojia, hivyo imewekeza kikamilifu katika ufundishaji wa kompyuta. Kila darasa hupata angalau vipindi viwili kwa wiki, vikifikisha zaidi ya vipindi 40 kwa mwaka kwa mwanafunzi mmoja, ili kuhakikisha wanafunzi wanahitimu wakiwa na ujuzi wa msingi wa TEHAMA.
Shule pia inatoa Mafunzo ya kilimo na bustani kupitia shamba darasa
Mafunzo ya mapishi kila Jumamosi kwa wanafunzi wote wa bweni na wa kurudi nyumbani pia wanapata Elimu ya kazi za mikono na stadi za maisha
Kupitia programu hizi, shule inalenga kuandaa mtoto asiye tegemezi, mwenye uwezo wa kujitegemea na kuelewa majukumu ya kijamii.
Mazingira Salama na Bweni la Kisasa
Shule ina miundombinu iliyojengwa kimkakati kwa ajili ya ustawi wa mtoto, ikiwemo
Mabweni yenye usalama na utaratibu wa milo mitano kwa siku, ikiwemo mlo wa matunda kila siku kwenye mlo wa jioni na imekuwa na madarasa ya kisasa
Uwanja mpana wa michezo, Huduma za afya shuleni
Anasema kuwa shule hiyo inapokea watoto kutoka mikoa mbalimbali kama Dar es Salaam, Mbeya, Singida na Mwanza husoma katika shule hii kutokana na mazingira yake yenye ubora wa juu
Mkurugenzi wa shule hiyo, Eunice Kimath anasema kuwa shule imekuwa ikiwasaidia Watoto wanaoishi katika Mazingira Magumu
Shule ina mpango maalum wa kusaidia watoto wenye changamoto za kijamii. Hadi sasa, zaidi ya watoto 50 wanalelewa na kusomesha kupitia mpango huu, ikiwa ni sehemu ya mchango wa shule kwa jamii.
Mwito Kwa Wazazi
Mkurugenzi wa shule, Bi. Eunice Kimath, anatoa wito kwa wazazi wanaotafuta shule yenye ubora, uangalizi wa karibu, malezi ya kitaaluma na kimaadili, wafikirie Good Victory English Medium School.
“Tunapokea watoto wa dini zote, kutoka sehemu zote za Tanzania. Tunalea mtoto kiakili, kimwili, kimaadili na kiufundi. Hapa ni mahali salama pa ukuaji wa mtoto wa Kiafrika.” anasema Kimath
Anamalizia kwa kusema kuwa Kwa misingi ya nidhamu, elimu bora, teknolojia, malezi na mazingira salama, Good Victory English Medium School imeendelea kuwa kielelezo cha ubora wa elimu nchini. Uwekezaji wake katika walimu, miundombinu na malezi umeifanya kuwa kivutio kikubwa kwa wazazi wanaotaka elimu yenye matokeo halisi.





