

Mbunge wa Mtama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amechangia mjadala katika Bunge la Kumi na Tatu, Mkutano wa Pili, Kikao cha Nne, kilichofanyika leo Februari 05, 2026.
Katika mchango wake, Nape aliibua hoja muhimu akiitaka Serikali kuzingatia suala la utu katika utekelezaji wa majukumu yake, hususan kwenye vyombo vya dola na katika kuwahudumia wananchi.
Alisisitiza kuwa utu unapaswa kuonekana kwa makundi mbalimbali ikiwemo kwa wafanyabiashara wadogo (machinga), wakulima pamoja na katika matendo ya vyombo vya dola, akionya kuwa kupuuza maadili hayo kunaweza kuathiri uaminifu wa wananchi kwa chama.
“Kwenye machinga kuwe na utu, kwa wakulima kuwe na utu, na katika matendo ya vyombo vya dola tuone utu. Tukimung’unya maneno, CCM itaondoka,” alisema Nape akichangia Bungeni.
The post ”Tuone Utu, Tukimung’unya Maneno CCM Itaondoka” – Nape – Video appeared first on Global Publishers.




