Na. Vero Ignatus, Arusha.
Mkutano wa tano wa serikali mtandao umefanyika Leo Jijini Arusha ambapo umewakutanisha Takriban wadau 1000 ambapo utafanyika kwa siku tatu, kuanzia kwa Leo 11februari-13 februari 2025 ukiwa na lengo la kujadiliana kuhusu hali ya utekelezaji wa Serikali Mtandao nchini
Akifungua kikao kazi hicho Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) amesema kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa Benki ya dunia ya mwaka 2022 iliyojumuisha nchi 198 duniani juu ya ukomavu wa matumizi ya teknolojia na utoaji wa huduma serikalini,ushirikishwaji wa wananchi ilibainishwa kuwa Tanzania imekuwa ikifanya vizuri , kutoka daraja kundi B hadi kundi A na kushika nafasi ya 26 duniani, ya 2 barani Afrika na nafasi ya 1 Afrika ya mashariki.
Dkt Mpango ameitaka mikoa ile ambayo haijajiunga katika mfumo huo ifanye hivyo kabla ya tarehe 30 June 2025 bila Kukosa, huku akimsisiatiza shughuli za e-GA zinaimarishwa na kupatiwa nafasi ya kipaumbele zaidi na kujenga mfumo mkubwa wa ili kuhakikisha mifumo ya serikali inasomana na kubadilishana tsarina.
“IPO mikoa mikuu 2 hawajaingia kwenye e office inasikitisha kwaajili ya kuwatunzia heshima yao naomba nisiitaje Ila tunawashauri wajiunge kabla ya 30 June 2025 bila Kukosa”. Alisema.
Awali akitoa salamu Mkurugenzi wa (e-GA)Mhandisi Benedict Benny Ndomba amesema kuwa kikao kazi hicho cha tano kutakuwa na mada 18 zitakazojadiliwa kwa Siku hizo 3 huku (e-GA) itawasilisha taarifa ya utekelezaji wa maazimio 12 yaliyofikiwa katika Mkutano wa nne (4) wa Serikali Mtandao uliofanyika Februari 2024.
Ndomba amesema kikao hicho Kimewakutanisha watumishi mbalimbali wakiwemo viongozi na watumishi mbalimbali wa sekta ya umma wakiwemo Makatibu Wakuu, Maafisa Masuuli, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na vitengo vya TEHAMA, Maafisa TEHAMA pamoja na Maafisa wa kada nyingine, huku lengo likiwa kuyakutanisha wadau katika taasisi na mashirika ya umma, ili waweze kujadili kwa pamoja jitihada mbalimbali za utekelezaji wa Serikali Mtandao, na kuweka mikakati itakayosaidia kukuza jitihada hizo.
Ameongeza kuwa, mkutano huo unatarajiwa kuongeza uelewa kwa washiriki kuhusu serikali mtandao, teknolojia mpya zinazoibukia sambamba na namna zinavyoweza kutumika katika kuimarisha utendaji kazi serikalini na kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa umma.
“Mkutano huo utaongozwa na kauli mbiu isemayo “Utekelezaji wa Jitihada za Serikali Mtandao na Ubunifu kwa utoaji wa huduma bora kwa umma” ikiwa na lengo la kuchochea ubunifu na utekelezaji wa Jitihada za Serikali Mtandao kwa Taasisi za Umma, ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa umma”, amesema Ndomba
Kwa upande wake Waziri wa nchi ofisi ya raisi menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora GeorgeSimbachawen (e-GA)ni kiunganishi cha kupeleka huduma kwa wananchi kwa urahisi ili wananchi wapate huduma stahiki kwa haraka bila kuwepo kwa vitendo vya rushwa vilevile kujadili kwa pamoja jitihada mbalimbali za utekelezaji wa Serikali Mtandao, na kuweka mikakati itakayosaidia kukuza jitihada hizo.
“Dunia ya leo e-GA ni kama muundo wa kurahisisha mifumo ndani ya serikali na utoaji huduma kwa urahisi katika mifumo ya serikali ,niwapongeze kwa hatua na malengo haya na mimi.kama kiongozi naridhika kuwa e-GA mmefanya kazi yenu sawasawa.” amesema Simbachawene.
Aidha Ameongeza kuwa lengo la kuandaa kikao kazi hicho ni kiwakutanisha wadau wa serikali mtandao katika.taasisi na mashirika ya umma na sekta binafsi ili kuwapatia fursa ya kujadili hatua iliyofikia katika utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao.
Mkutano wa tano wa serikali mtandao ambapo umewakutanisha Takriban wadau 1000 ukiendelea katika Kituo cha mkutano cha AICC Jijini Arusha Leo 11februari 2025
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akiwasili kwenye kikao kazi cha tano cha Serikali mtandao, kinachofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Dkt. Philip Mpango amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda.
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akiwasili kwenye kikao kazi cha tano cha Serikali mtandao, kinachofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).hapa akisalimiana na Waziri wa nchi ofisi ya raisi menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA)Mhandisi Benedict Benny Ndomba kuzungumza katika kikao kazi cha tano kilichofanyika Jijini Arusha Leo 11 februari2025
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Kuwe Bakari
Kutoka kulia ni Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akimkabidhi tuzo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Kuwe Bakari