Serikali ya Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro imesema imeanza mchakato wa kukarabati uwanja wa Ndege Tende uliopo Wilayani humo ikiwa ni mikakati ya kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amesema uwanja huo Kwa Sasa umeacha kutumika.kwa zaidi ya miaka 30 hivyo katika kuimarisha shughuli za Utalii katika hifadhi ya Taifa Mikumi Serikali imekusaidia kuufufua uwanja huo.
Amesema uwanja huo utakuwa na urefu wa Kilometa 5.4 na pia utakuwa na uwezo wa kupokea Ndege za aina zote kubwa na ndogo.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hasan amekweza miundombinu mbalimbali kwenye sekta ya utalii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Kilosa Wilfred Sumari amesema kuanza Kutumika Kwa uwanja huo utasaidia Kuongeza watalii katika hifadhi ya Taifa Mikumi na kufungua fursa mbalimbali za kichumi na uwekezaji kwa wakazi wa Wilaya hiyo.
Amesema Reli ya kisasa ya SGR na uwanja huo wa ndege umekuja kuleta matumaini mapya ya Wilaya ya Kilosa kwenye sekta Usafiri na usafirishaji.
Nao wakazi wa Kata ya Magomeni Wilaya humo wameipongeza Serikali Kwa hatua hii nakuamini kuwa utasaidia kurahisha Usafiri wa anga na kuitangaza Kilosa.
Wamesema miaka ya nyuma uwanja huo ulivyokuwa ukifanya kazi ulisaidia Kuongeza kipato Cha wakazi wa eneo hayo hasa kuuza vitu mbalimbali ikiwemo zao la mkonge.
The post Serikali Kilosa Kufufua uwanja wa Ndege. first appeared on Millard Ayo.