Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imefanya ziara ya kikazi katika mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu na kupongeza jitihada zinazofanywa na mgodi kujali afya za wafanyakazi wake na jamii nzima ya vijiji vinavyozunguka mgodi huo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hassan Mtenga akiongea baada ya kuhitimisha ziara hiyo amesema Kamati imeridhishwa kwa jinsi mgodi unavyotekeleza programu za afya za ndani na nje hususani katika kupambana na UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu na magonjwa mengineyo yanayoweza kusababishwa na shughuli za uzalishaji mgodini.
“Katika wasilisho lenu tumeona ni jinsi gani kampuni ya Barrick iko mstari wa mbele kulinda afya za wafanyakazi wake na jamii nzima ya maeneo yanayozunguka mgodi na kwa jinsi inavyofanikisha miradi ya Afya kupitia fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) pia tumefurahi kusikia asilimia kubwa vya wafanyakazi katika migodi ya Barrick hapa nchini ni watanzania”,amesema Mtenga.
Kwa niaba ya Kamati, Mtenga ametoa pendekezo kwa Mgodi wa Barrick kuangalia uwezekano wa kuchangia Mfuko wa Taifa wa UKIMWI, pendekezo ambalo uongozi wa Mgodi umesema utalifanyia kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa na Wilaya kupitia Kamati za Maendeleo ya jamii.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesema uendeshwaji wa migodi ya Barrick ambayo ina ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals ni wa weledi mkubwa na viwango vya kimataifa, uwazi ,unazingatia sheria za nchi na ni kielelezo cha uwekezaji wa kupigiwa mfano katika sekta ya Madini nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amepongeza Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuhakikisha wakati wote unafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Serikali sambamba na kufanikisha miradi mikubwa ya maendeleo katika mkoa hususani katika sekta za elimu, afya, maji na ujenzi wa miundo mbinu ya barabara.
Awali akitoa taarifa kwa Kamati hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Victor Lule amesema kuwa mgodi umekuwa mstari wa mbele kuendesha programu za kudhibiti maambukizi ya UKIMWI na Malaria kwa wafanyakazi wake pia umeimarisha zahanati ya mgodi kuhakikisha inatoa huduma bora na za kisasa wakati wote.
Lule ameongeza kuwa mbali na kuimarisha huduma za ndani ya Mgodi pia mgodi umekuwa mstari wa mbele kuboresha kituo cha afya cha Bugarama na kupeleka kampeni ya kupambana na Malaria ijulikanayo kama Zero Malaria kwenye vijiji vinavyozunguka Mgodi kwa kupuliza dawa za kuua mazalia ya mbu na kuwagawia wananchi vyandarua vyenye dawa.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS, Dkt. Catherine Joachim ametoa ushauri kwa Mgodi kuendesha programu za tohara kwa wanaume na dawa za kuzuia maambukizi mapya ndani na nje ya mgodi na kuongeza kuwa licha ya kuwepo madawa ya kufubaza virusi vya UKIMWI bado kuna maambukizi mapya yanaendelea kujitokeza na sehemu mojawapo hatarishi kupata ugomjwa huo ni maeneo ya migodini.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI wakitembelea Zahanati ya mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya, UKIMWI Mhe. Hassan Mtenga akizungumza wakati ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa akizungumza wakati ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Victor Lule akizungumza wakati ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu
Mkuu wa Mahusiano ya Jamii na Mazingira Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Agapit Paul akizungumza wakati ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI katika mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu