Na. Vero Ignatus,Arusha
Wizara ya fedha kupitia kamati ya ushauri ya sera ya za kodi imesema maandalizi ya kongamano la Kitaifa la kodi mwaka 2025 limepangwa kufanyika Jijini Dar es salaam aprili 15 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, washiriki zaidi ya 1000 kutoka sekta ya umma ,na binafsi,huku mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Isdory Mpango,ambapo azma ya kogamano hilo linalenga kuongeza ukuzaji wa rasilimali za ndani kwa kustawisha fursa za wananchi pamoja na kujadili hatma ya nchi kwa ujumla.
Akizungumza Leo tarehe 10/4/2025 na waandishi wa habari Jijini Arusha juu ya kongamano hilo Naibu Katibu mkuu Wizara ya Fedha Elijah G Mwandumbya amesema kutakuwepo wadau na wataalam mbalimbali waliofanikiwa katika shughuli zao ,watakaowasaidia kuwaeleza jinsi wanavyojifunza na hatua gani muhimu wazichukue ili nchi ikue kiuchumi ipasavyo huku wananchi wakiaswa kutumia fursa hiyo iliyotolewa na serikali kwa kila mmoja kutoa maoni na kuwasilisha ili kuweza kuboresha sera za kodi.
‘’Mtakumbuka ndugu wananchi kuanzia 2021 wakati Mhe. Dkt Samia alivyoingia madarakani na kupitia uanzishwaji wa kongamano kama hili hatua mbalimbali zimechukuliwa ambazo zimepelekea mafanikio makubwa katika uchumi wetu na sisi tunaona mafanikio hayao muhimu sana kuonyesha kwamba nchi yetu ipo kwenye njia sahihi katika maeneo mbalimbali hivyo basi ni vyema kutumia mafanikio haya kujenga mafanikio zaidi kwa wananchi ’’alisema
Mwandubya amesema mwaka 2022 kupitia sera ambazo waliweza kuzirekebisha miradi zaidi ya 293 iliweza kusajiliwa na kituo cha uwekezaji Tanzania,ambapo ilikuwa na thamani ya trilioni 11.7,Mwaka 2023 miradi 526 ilisajiliwa yenye mitaji ya shilingi trilioni 14.6 ikiwa na matukio mbalimbali ya kuweza kupata ajira mapato kwa wananchi,mwaka 2024 peke yake miradi nyenye thamanai ya trilioni 24.67ambayo ni miradi 901 imesajiliwa kupitia kituo hicho, matokeo yake ni sera ya awamu ya 6 zimewezesha kufungua uchumi kwa wananchi kutoka ndani na nje ya nchi wanashiriki kwenye ujenzi wa uchumi.
Aidha alisema kuwa mafanikio ambayo yametokana na sera hiyo alisema kuwa mapato ya ndani mwaka 2022-23 yalikuwa shilingi trilioni 26.7 lakini Mwaka 2023-24 mapato hayo yalikuwa shilingi trilioni 29.8 kwa kipindi cha kuanzia julai 2024 hadi februari 2025 mapato hayo yameweza kufikia shilingi trilioni 22.5,hivyo hatua za ukusanyajiwa mapato zinatokana na shughuli za kiuchumi ambazo zinafanywa na wananchi/vilevile kukua kwa ukusanyaji wa mapato kunatokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi .
‘’Kwamfano mwaka huu wa fedha taasisi yetu ya mamlaka ya mapato TRA imefanikiwa kukusanya kuanzia julai –machi 2025 imeweza kufanikiwa kukusanya zaidi ya 100%ya malengo ambayo imewekewa kwahiyo hiyo inakwambia ya kwamba shughuli za kiuchumi zinakwenda vizuri kitu kingine ule ushawishi na mikakakti ya ukusanyaji wa mapato ni rafiki na inawezesha shughuli za wananchi kukua kiuchumi viziri zaidi’’alisema.
Vilevile ameainisha kuwa Sekta ya fedha kuwa na mchango mkubwa katika ukusanyaji wa mapato kwa namna inavyoendesha na kushiriki,ikifuatiwa na sekta ya Madini,ambapo serikali inaendelea kukuza uwezo wa taasisi hizo,Viwandani,kampuni za wamawailiano pamoja na zile zinazoshiriki katika kuuza na kununua,pamoja na mchango mkubwa wa sekta hizo kwenye ukusanyajin wa mapato ,mchango mwingine mkubwa ni wa kukuza na kuiendeleza jamii kupata huduma bora zaidi .
Mwaka 2023 serikali kupitia wizara ya fedha ilianzisha maadhimisho ya siku ya kongamano la kodi kitaifa ikiwa ni ushirikishwaji wa wananchi katika hatua za kupokea mapendekezo wa mfumo wa kodi nchini ambapo maandalizi ya kongamano la kitaifa la kodi 2025 yalianza kikanda yaliyofanyika kuanzia tarehe 18novemba 2024 -6dec 2024, yalifanyika katika kanda za mashariki,kaskazini,kanda ya ziwa kanda ya magharibi,kanda ya Kati, kanda ya nyanda za juu kusini pamoja na kanda ya kusini.
‘’Kazi yetu ni kuwafikia wananchi,wafanyabiashara wadau mbalimbali kwenye maeneo ambayo katika kuhakikisha kwamba tunakusanya maoni yatakayofaa kwaajili ya maendeleo ya nchi yetu pale ambapoyatakuwa yamefanyiwakazi na kupelekwa bungeni na kufanyiwa kazi na kuwa sheria zinazotuongoza katika utekelezaji wa majukumu lakini pia katika ufanyaji wa biashara.
Naibu Katibu mkuu Wizara ya Fedha Elijah G Mwandumbya kizungumza Leo tarehe 10/4/2025 na waandishi wa habari Jijini Arusha juu ya kongamano la Kodi litakalofanyika Jijini Dar es salaam aprili 15 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.