Na Issa Mwadangala.
Polisi Kata ya Mwakakati Wilaya ya Momba Mkoani Songwe Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Robart Philipho amewataka wajasiliamali wanaofanya shughuli za ususi na mapambo kuacha tabia ya kuwa chanzo cha migogoro ya kifamilia.
Mkaguzi Robert alitoa kauli hiyo Aprili 24, 2025 wakati akitoa elimu ya madhara ya migogoro katika jamii na familia ambapo aliwaeleza wajasiliamali hao kuacha tabia hiyo ambayo imekuwa ikiota mizizi siku hadi siku na kusababisha madhara makubwa katika familia na jamii suala ambalo si zuri katika maisha ya mwanadamu.
“Siku zote migogoro inarudiaha nyuma maendeleo na ustawi wa familia basi sitopenda kusikia ndani ya kata yangu kuna migogoro ambayo inayoweza kuepukika” alisema Mkaguzi Robert.
Aidha, Mkaguzi Robert aliwaomba wajasiliamali hao kuzingatia mazungumzo yao wanapokuwa wanawasiliana na wateja wao wakiwa wanawahudumia ili kuondoa changamoto hiyo katika eneo lao la kazi.
Sambamba na hayo aliwaomba wajasiliamali hao kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kuhusu uhalifu na wahalifu ili kata hiyo iendelee kuwa shwari muda wote.