Wasanii wa filamu na maigizo nchini wametakiwa kutumia Lugha ya kiswahili kama fursa ya kibiashara kimataifa ili kuongeza tija itokanayo na filamu hizo katika kujiongezea kipato chao
Rai hiyo imetolewa na Dkt Godwin Maimu ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa tamasha la kimataifa la filamu za kiswahili (ISFF) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam ambapo amesema lengo la kuanzisha tamasha hilo ni kubidhaisha lugha ya kiswahili kimataifa kupitia filamu za kiswahili zitakazoonyeshwa katika mataifa mbalimbali.
Kwa upande wake mchunguzi lugha mkuu kutoka baraza la kiswahili Tanzania (BAKITA) amewasisi wasanii nchini Kutumia lugha ya kiswahili kwa ufasaha ili kulinda hadhi ya lugha hiyo huku wakiendelea kuutangaza utamaduni wa kitanzania kimataifa
Naye Dusabimana Apollos msanii kutoka nchini Rwanda amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kwa wasanii wa afrika mashariki katika kukuza matumizi ya lugha ya kiswahili hususan katika masoko ya kimataifa